Ni kweli haki yenu watu MILIONI MOJA (1,000,000) italindwa na mtapata haki sawa AS LONG AS MTAHESHIMU SHERIA ZA NCHI. Vinginevyo, sheria na taratibu za nchi za kushughulikia waleta fujo wachache zitafuatwa. Hili halina mjadala wala hoja kwani ni utaratibu wa KIDUNIA; hata huko Ughaibuni utaratibu ni huo huo, haijarishi ulikuwa mgombea au mpiga kura. Halafu, ni utaratibu gani huu ulioibuka siku hizi!? Mtu akitishiwa tu na mlevi mwenzake huko kwenye ulevi, basi anaibuka na kusema nimetishiwa maisha na KUKIMBIA NCHI! Hiki ni nini jamani, mbona sielewi!? Mtakimbia wangapi!? Hata huko unakokimbilia watastuka jamani!