Ni zipi sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Best Student Chuo Kikuu?

je iyo 4.7 ni kwa wastani wa miaka yote mitatu/minne?

habari chini ya kapeti, inabidi iwe above or equal 4.8
Chini ya kapeti nyingine, GPA iwe inapanda au kubaki CONSTANT... mambo ya leo una 4.9 halafu kesho una 4.8, huko ni kushuka hata kama umeshuka kwa juu, bado umeshuka tu..!! na hata kama inayofuata ni 5.0 bado umeyumba.. eidha upige 4.9, then 4.9 then 4.9 AU 4.8, 4.8 na umalizie na 5.0 AU 4.8, 4.9, 4.9, 4.9...
 
Hesabu za wastani ulipata ngapi.
 
Mkuu mbona mnapotosha? GPA inakuwa calculated based on raw marks, hiyo ndiyo system. Mwenye GPA kubwa maana yake alikuwa na raw marks za juu.
 
Si kweli mkuu, kasome vizuri tena. GPA inakuwa calculated kwa raw marks.
 
1)Nipe faida tatu unazozipata
2)Una Address inayofahamika
3)Gross Worth n Net??
aja ujinga kwani wote walio jiajiri hapo mtaani kwako wana address, wanaweka faida zao hadharani, hata ukichukua gunia la mpunga shambani na kwenda kuliuza hapo pia umejiajiri.
 
aja ujinga kwani wote walio jiajiri hapo mtaani kwako wana address, wanaweka faida zao hadharani, hata ukichukua gunia la mpunga shambani na kwenda kuliuza hapo pia umejiajiri.
Huna Address wewe ni unaganga njaa Mkuu.
 
Mkuu mbona mnapotosha? GPA inakuwa calculated based on raw marks, hiyo ndiyo system. Mwenye GPA kubwa maana yake alikuwa na raw marks za juu.

Kwa mujibu wa Prospectus, uzoefu wangu na uhalisia wa mambo, as far as UDSM is concerned, maelezo yangu hapo juu yapo sawa, sawia na sahihi.

Ngoja tuelezane kwa mifano.
Raw marks kuanzia 70 hadi 100 ni alama A.
Kwahiyo mwenye 71 na mwenye 98 wote wana A.

Chukulia wanafunzi wawili, wamesoma masomo 40 kwa miaka yote mitatu (semista 6).

Matokeo ya mwanfunzi wa kwanza:
Amepata kila somo marks 70, kwahiyo ana A zake 40.
Raw marks zake ni 70x40 = 2800
Ila kwa sababu amepata A zote, basi mtu huyu ana GPA ya 5.0

Matokeo ya mwanfunzi wa pili:
Amepata marks 100 kwenye masomo 37
na yale matatu yaliyobakia amepata marks 60.
Huyu mtu ana A zake 37 na B+ zake 3.
Raw marks za mtu huyu ni 37x100 = 3700
Jumlisha 3x60 = 180 ambapo unapata 3880 (Kumbuka yule wa kwanza ana 2800)

GPA ya mtu huyu ni around 4.9 (Kumbuka yule wa kwanza ana 5.0)

All day, everyday, mtu mwenye GPA ya 5.0 anakua best and superior kwa yule mwenye 4.9 hata Kama anazidiwa ''Raw Marks''

Nilichoeleza hapo juu ni kwamba Kama itatokea watu wamelingana GPA, na anatafutwa mkali mmoja zaidi ya mwingine, then wanaenda kuangalia ''Raw marks''
Kama ni kwenye soka, tunasema watu wakifanana points, tunaenda kuangalia ''Goal differences''.

NB: Hoja yako (ya kwamba GPA inakokotolewa directly kutoka kwenye Raw marks) itakua na mashiko endapo tutaizungumzia grading system ya Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA).

Niko tayari kutuma them most recent undergraduate prospectus ya UDSM, kipengele kinachozungumzia grading system, ili nithibitishe madai yangu, kama utataka nifanye hivyo.

Karibu.

 
We ndo kiazi , kwamba University of Dar es salaam Best Students wote wanapaswa kwenda BOT kila mwaka hata kama katoka kozi ya petroleum au engineering. Soma alichoandika huyo niliyem-quote sio unakurupuka mkuu.

Hivi ni lazima mchangie kila uzi dah...kwahiyo ndo kirefu cha UDBS hicho [emoji3][emoji3][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…