Niache kazi Serikalini niende Botswana? Naomba ushauri

Sasa km hili unalijua, shida iko wapi? Si ndo ufanye hayo maamuzi sahihu kadri ya hitaji lako.
Nimeleta jukwaani kupata maoni ya wadau na watu wenye experience nisije kuacha hapa nikaenda huko mambo yakawa mabaya na nishaharibu huku najua hapa jukwaani kuna wadau pia wanafanya kazi huko Botswana maana naskia wabongo wapo wa kutosha tu huko Gaborone
 
Oooh bas sawa, subiri wanakuja kukupa ufafanuzi na muongozo.
 

Kama una kazi Bongo, usiache na kwenda Nchi za watu kwa mshahara wa 2.1m hiyo hela ni ndogo sana kwani kwa wenzetu maisha yapo juu.
Angalia mwenyewe ILA usiache kazi, hiyo hela hailipi!
Nyongeza; Ukitaka kusaini mkataba wa kufanya kazi nje ya nchi
Angalia sana mkataba ujumuishe vitu vifuatavyo (#1 &2&3) ni muhimu sana;
1. Bima ya Afya (Ogopa sana kuumwa ugenini halafu huna bima)
2. Makazi/nyumba
3. Working permit
4. LIKIZO pengine na nauli ya kukurudisha kwenu mara moja kwa mwaka
5. Angalia pia working hours ziwe wazi (usije kufanyishwa kazi masaa 16)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…