"Niambie", hili neno jibu lake sahihi ni lipi hasa?

"Niambie", hili neno jibu lake sahihi ni lipi hasa?

Kidedya

Member
Joined
Feb 24, 2020
Posts
56
Reaction score
37
Ndugu mabaharia na maharia, kama title inavosomekahapo juu, hilo neno kwangu limekuwa ni kitendewili sana hasa ninapokuwa nachati na marafiki wakike.

Unakuta unamsalimia anakujibu, halafu baada ya hapo zinaanza kumiminika izo 'Nambie'

Yaani kila baada ya neno, itafuata nambie, ukijibu unaambiwa tena nambie, unajibu unaambiwa nambie. Sielewi huwa nakosea kujibu au la

Nimelileta kwenu kama na ninyi ni wahanga basi tupeane uzoefu kimtindo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom