"Niambie", hili neno jibu lake sahihi ni lipi hasa?

Neno nambie mnalipenda sana wanaume aisee linaboa sana.kama MTU namheshimu akisema nambie majibu poa. Tofauti na hapo sijibu.
 
me manz angu alikua nayo an anaeza akuambie niambie had akuambie tena an ndan ya dakika tano umepikwa niambie kama kumi nikawa kila akiniambia niambie natulia, nikaja kumchana kuwa akiniambia niambie huwa nakausha manake alikuja kukomplain mbn sijibu text
hyo niambie inaboa kama zile za kutumia x badala ya s
 
mtu akiniabia hilo neno niambie ndio end of conversation, sijibu chochote tena.
 
Itakuwa ameweka auto reply

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wale wanaoandika vifupi, wananikera sana yaani.

Sana anaandika xn,
Poa anaandika p,
Tuonane anaandika 2o8,
Nakuja anaandika nkj.

Mm nawaambia kabisa sikuelewi.
Dadek niko na penzi jipya sasa kila akituma text ni zahivyo nishamchana sielewi ila bado anatuma sasa hivi najipanga upya akituma ya namna hiyo ni kumtwangia simu tu sina mda wa kupoteza habari za kuchat nadhani zimemshinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na hongera ila mbadilishe taratibu tu atazoea.

Mpe salam zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…