Niamini..Usitoe Code ya Biashara Yako...!

Niamini..Usitoe Code ya Biashara Yako...!

Biashara ni siri..aisee usitoe code kabisa

Mimi kuna biashara nilikua nafanya 7years back sasa bana nikampa code wife...wife ana rafiki yake si ampa siri yote!
Nakuja ingiza mzigo sokoni aisee! Soko Limejaa..nikabaki najiuliza
Nikatumia umafia sana nikajua ni yule dem na mumewe
Nika mbana yule dem si ndio aliniambia wife ndio alimwambia aisee ilikua balaa
......ila baadae waliishindwa na baadae ikawa sio deal tena
Ila nilijifunza..
Sa hivi code yangu ni yangu!
Umechelewa sana kujua hili. Hata hapa JF ukiona mtu kaja na code ya biashara na anashawishi watu wajiunge basi ujuwe kuwa anatafuta watu wa kupiga. Nina maana kuwa hakuna anayetoa siri ya biashara anayofanya. Pengine huyo mke wako ulikuwa hujamfundisha? Au wale ambao hawana siri, kwao mume ni mtu baki, lakini shoga ndiye muhimu?
 
Hakuna cha code wala ujinga gani, hakuna kipya chini ya jua. Kila kitu ni Consistency tu unaweza pewa hizo code na usifike mbali kama ukikosa Consistency na nidhamu
Ndio maana wao waliishindwa hiyo biashara...ila walinicost sana
 
Back
Top Bottom