Nichagulieni gari kwa bajeti ya Milioni 10

Ngoja madalali wakufuate PM, watakung'ang'ania hadi utajuta kutoa tangazo, hafu wengi gari ni vimeo kuwa makini
Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Udochi naona kuna watu wanakushauri vizuri wengine vibaya. Sasa fuata ushauri wangu.
Toyota Ist 1490cc itakufaa kwa sababu kwanza bajeti yake ndio hiyo milioni 9.5 mpaka 10.5m
Kwa ulaji wa mafuta utaiweza na Ac pia unawasha.
Kwa vile ni mjasiriamali hata bidhaa zako za dukani unaweza kununua kutoka labda pale kwa Moshiro Kinyerezi kuzipeleka huko mjini kwako unakouzia bila tabu na petrol ikatumika ya wastani tu.
Usinunue Noah, Brevis, Mark 2 Grande zitakufilisi wala Vitz pia usinunue.

Na hiyo Ist mil 9.5 mpaka 10.5 unazipata hapahapa Dar wala usihangaike kuagiza.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watafutwe kimomwe motors watakuchagulia na kukuagizia gari safi.wapo Facebook, tweeter, ofisi ziko magomeni mapipa, pembeni ya stand ya mwendokasi upande wa kulia ukiwa unaelekea kariakoo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…