Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
"Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko tangu umeteuliwa malalamiko ya Umeme yanapungua. Nakupongeza sana! Mvua zilizonyesha Jimbo la Mbogwe watu wameporomokewa na majumba, wengine wamelazwa Hospitali ya Masumbwe, Nitoe pole kwa Wananchi Mungu awajalie"
"Wilaya ya Mbogwe bado nina vitongoji 196 ambavyo vinahitaji Umeme. Nikuombe Waziri wa Nishati unisaidie sana ili wananchi waweze kupata Umeme kwenye hii bajeti ya Trilioni 1.8. Ukanda wetu tunalima mazao, mashine za kusaga na Makrasha wanahitaji huduma ya Umeme. Majimbo ya Bukombe na Mbogwe hatuna Transfoma. Tunaomba Mtenge Transfoma ili umeme utulie"
"Wilaya ya Mbogwe tuna Vijiji 87. Namshukuru Mheshimiwa Rais vijiji vyote vimefikiwa na Umeme. Naomba wabunge tupitishe hii bajeti bila wasiwasi. Mwaka 2023 tulikwenda nchi ya India 🇮🇳 na Ethiopia 🇪🇹 kuhusu sekta ya Nishati. Yanayowezekana India hata Tanzania 🇹🇿 Yanawezekana"
"Niombe Serikali itoe fedha haraka za bajeti maana sekta ya Nishati ni moyo wa Taifa letu. Waziri wa Nishati wasimamie ipasavyo kukomesha suala la upandaji holela wa Mafuta. Mpaka sasa Lita ya Mafuta ni Shilingi 3000+ na maisha yanazidi kuwa magumu. Sasa Umeme ni wa kutosha mfikirie kupunguza bei kwenye Unit pamoja na kuwaunganishia watu Umeme"
"Vipo vijiji tunavipelekea Umeme kwa Shilingi 300,000. Naiomba Serikali iangalie upya turudi kwenye Shilingi 27,000 kama zamani. Transfoma zilizopo Masumbwe, Lulembela, Lugunga ni kidogo. Tunaomba Transfoma zingine kama zilikuwepo za 50W basi ziende za 100W ili wananchi wapate huduma nzuri ya Umeme Mbogwe".