Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicole Joyberry kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufanya biashara ya kuanzisha ma-group na kukusanya pesa kinyume na sheria.

Soma pia: Nicole Berry, mwanadada anayepiga mamilioni kwenye kilimo cha vitunguu Iringa

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro na kusema matukio hayo yametokea katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wakati mwingine nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Your browser is not able to display this video.

"Matukio haya yametokea ndani na nje ya Dar es Salaam, kwa kuhamasisha baadhi ya watu akianzisha ma-group mbalimbali na kuweka majina hewa kwenye ma-grouup hayo kwamba wanachangia pesa na baada ya muda mfupi basi utapata kiwango kikubwa cha pesa, jambo ambalo baadaye anakuja kutopatikana kwenye simu na kupotea na pesa ambazo watu wamechangia," amesema Kamanda Muliro





 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…