Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Attachments

  • 1741189043833.jpg
    1741189043833.jpg
    305.1 KB · Views: 1
  • 1741189042517.jpg
    1741189042517.jpg
    390 KB · Views: 1
Wakuu,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicole Joyberry kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufanya biashara ya kuanzisha ma-group na kukusanya pesa kinyume na sheria.

Soma pia: Nicole Berry, mwanadada anayepiga mamilioni kwenye kilimo cha vitunguu Iringa

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro na kusema matukio hayo yametokea katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wakati mwingine nje ya mkoa wa Dar es Salaam.


"Matukio haya yametokea ndani na nje ya Dar es Salaam, kwa kuhamasisha baadhi ya watu akianzisha ma-group mbalimbali na kuweka majina hewa kwenye ma-grouup hayo kwamba wanachangia pesa na baada ya muda mfupi basi utapata kiwango kikubwa cha pesa, jambo ambalo baadaye anakuja kutopatikana kwenye simu na kupotea na pesa ambazo watu wamechangia," amesema Kamanda Muliro

Kama unaikumbuka ile nyimbo ya sumalee hakunaga yule video kile kidem jamaa alikua anakibembeleza na kucheza nako ndio huyu kwa sasa"
 
Hua nafurahi sana kuona watu wanatapeliwa kwa style kama hizo, mpumbavu mmoja anamuamini mtu kisa ana mataco makubwa basi 😂

Yule nabii wa Congo amewanyoosha watu, na bado kuna watu wa kanisani kwake wakawa wanamtetea tena hadi kwenye vyombo vya habari 🙌 aisee sisi watanzania ni wapumbavu mno na bado wapumbavu wataendelea kunyooshwa.
 
Kama unaikumbuka ile nyimbo ya sumalee hakunaga yule video kile kidem jamaa alikua anakibembeleza na kucheza nako ndio huyu kwa sasa"
Dah em ngoja niingie YouTube aisee dah 🙌 kama n yeye kweli bc acha watu wawe matapeli tuu mana kwa mwili ule afu now ana mwili huu wa sasa bc sio poa kuuhudumia n lazima uwe tapeli na malaya🔥
 
Back
Top Bottom