Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Hii habari JamiiForums wanaificha jukwaa la ma Celebrities, je ni JamiiForums robot ndiyo imefanya chaguo hili?

Inabidi uongozi wa JamiiForums kuchukua hatamu za maamuzi badala ya kuliachia Robot kufanya maamuzi uzi muhimu kama huu kutupwa na kufichwa katika vichochoro vya jukwaa la Celebrities
 
Wakuu,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicole Joyberry kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufanya biashara ya kuanzisha ma-group na kukusanya pesa kinyume na sheria.

Soma pia: Nicole Berry, mwanadada anayepiga mamilioni kwenye kilimo cha vitunguu Iringa

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro na kusema matukio hayo yametokea katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wakati mwingine nje ya mkoa wa Dar es Salaam.


"Matukio haya yametokea ndani na nje ya Dar es Salaam, kwa kuhamasisha baadhi ya watu akianzisha ma-group mbalimbali na kuweka majina hewa kwenye ma-grouup hayo kwamba wanachangia pesa na baada ya muda mfupi basi utapata kiwango kikubwa cha pesa, jambo ambalo baadaye anakuja kutopatikana kwenye simu na kupotea na pesa ambazo watu wamechangia," amesema Kamanda Muliro

TABU MBAGA
 

Attachments

  • 30295cb781b9b3a97b0037fd12bfe3d2.mp4
    1.5 MB
Back
Top Bottom