NIDA wanapataje hela za kutoa gawio kwa serikali?

NIDA wanapataje hela za kutoa gawio kwa serikali?

kwenye investments zenye permanent establishment, usiwe na mashaka, (hapa inaonyesha hata tungekuwa tunaibiwa au tuliibiwa poa tu et?),
OSHA Kila mwaka wanafanya ukaguzi usio bure na wa lazima kwa kila taasisi waliyoisajili, mbali na gharama za usajili wa eneo la kazi jipya (taasisi)
Mkuu, hivi kweli tozo pekee ndio zinaweza fikia fedha nyingi kiasi cha kuwawezesha kutoa gawio la 5.38 Billions..!!??
Hii inanipa wasiwasi kwamba sasa kama hivyo ndivyo, basi OSHA kazi yao sio kutowa elimu ya Usalama na Afya sehemu za kazi, bali imebadilika na kuwa idara ya faini kwa makosa ya Usalama na Afya sehemu za kazi.
Mkuu, hata kama OSHA wanatowa mafunzo kwa malipo ya watahiniwa, lakini bado naona hicho kiasi bado ni kikubwa sana
 
IFM ni chuo kilicho chini ya wizara ya fedha, kuna uwezekano mkubwa mishahara inalipwa na serikali hivyo huwa na ziada ya kutosha ya fedha za kupelek hazina
Ziada inatoka wapi sasa? Kwenye Ada? Au chuo kinafanya biashara?
 
IFM ni chuo kilicho chini ya wizara ya fedha, kuna uwezekano mkubwa mishahara inalipwa na serikali hivyo huwa na ziada ya kutosha ya fedha za kupelek hazina

Utakuwa hujui maana ya Gawio
 
Hizi Taasisi zitaanza kutoka kwenye malengo yake ya kuanzishwa endapo zitalazimishwa kuwaza Gawio kila mwaka.

Badala ya kutoa elimu zitaanza kukomaa kutoza faini, kubana mambo ya kiofisi kama kuongeza uwezo kwa wafanyakazi n.k
kwenye investments zenye permanent establishment, usiwe na mashaka, (hapa inaonyesha hata tungekuwa tunaibiwa au tuliibiwa poa tu et?),
OSHA Kila mwaka wanafanya ukaguzi usio bure na wa lazima kwa kila taasisi waliyoisajili, mbali na gharama za usajili wa eneo la kazi jipya (taasisi)
 
Sijaona ttcl mwaka huu??? Vipi ATCL nayo, tuliambiwa Kuna ka faida kamepatikana mbona hawajatoa gawio???? Boss jana kasema kama hawana wauze hata magari yao ili mradi watoe gawio
 
NHC IMENISTAAJABISHA SANA KWA NINI MCHANGO WAO NI KIDUCHU MNO?,LAZIMA KUNA WALAKINI HAPO.SI BUREE .....!
 
Aloo hili swala lina hitaji ufafanuzi .Almost wakati mimi nafatilia kitambulisho huduma zilikuwa bure au sasa hivi kuna malipo.?
 
Yani sijaona ya kufikisha 5.2B , mmepika tu midata
Je unajua kazi za OSHA au unataka kubisha tu. Ninazozijua Mimi ni kuna Registration fees( Inategemea na mtaji wa kampuni). Training fees ambayo ni mandatory kwa kila kampuni( katika kila wafanyakazi 13 anatoka mmoja, train za fire, electrical defects, health and safety, first aid na kadhalika) laki 500,0000 kwa kila mfanyakazi mmoja anae attend. Agronomic fees( unalipa kampuni kila mwaka kwa ajiri ya inspection ya OSHA mfano mtaji ukiwa milioni 200 basi wastani wake ni laki 9 hadi milioni 1 kwa mwaka. Penalties hapo ndo usiseme. Kwa hiyo OSHA wana hela kwelikweli.
 
IFM nayo imetoa gawio la 2 billion?

Dunia nzima Public University zinaendeshwa kwa ruzuku ya Serikal na zile Ada ni sehemu ndogo tu
Usikariri ndugu, vyuo vyote ambavyo viko chini ya Taasisi za Serikali ziliruhusiwa kujiendesha zenyewe kwa Faida tangu kipindi cha Mkwere kasoro vyuo vichache tu vinavyohudumiwa na Serikali kuu
 
Usikariri ndugu, vyuo vyote ambavyo viko chini ya Taasisi za Serikali ziliruhusiwa kujiendesha zenyewe kwa Faida tangu kipindi cha Mkwere kasoro vyuo vichache tu vinavyohudumiwa na Serikali kuu

Unajiendeshaje kwa Faida wakati wote Mishahara inalipwa direct kutokea utumishi/Hazina?

Au neno kujiendesha kwa faida hujui?
 
Nadhani wanakosea kuita gawio, makampuni kama Nida na TPA na mengine ya aina hiyo yanabanwa na finance act nadhani ya 2013 inayoyataka kutoa 15% ya gross income kwenda hazina
 
Mfano ifm na udsm ikiwakilisha vyuo.......udsm tu 2017 ilipata ruzuku bilioni 78 toka serikalini ,ada bil 34 ,mishahara tu bil 80 ,bila ruzuku hawabaki na kitu.........gawio watoe wakati hawajitosherezi ?au tuite return tu
 
Attachments

  • Screenshot_20191126-001132.png
    Screenshot_20191126-001132.png
    43.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom