NIDA wanapataje hela za kutoa gawio kwa serikali?

kwenye investments zenye permanent establishment, usiwe na mashaka, (hapa inaonyesha hata tungekuwa tunaibiwa au tuliibiwa poa tu et?),
OSHA Kila mwaka wanafanya ukaguzi usio bure na wa lazima kwa kila taasisi waliyoisajili, mbali na gharama za usajili wa eneo la kazi jipya (taasisi)
 
IFM ni chuo kilicho chini ya wizara ya fedha, kuna uwezekano mkubwa mishahara inalipwa na serikali hivyo huwa na ziada ya kutosha ya fedha za kupelek hazina
Ziada inatoka wapi sasa? Kwenye Ada? Au chuo kinafanya biashara?
 
IFM ni chuo kilicho chini ya wizara ya fedha, kuna uwezekano mkubwa mishahara inalipwa na serikali hivyo huwa na ziada ya kutosha ya fedha za kupelek hazina

Utakuwa hujui maana ya Gawio
 
Hizi Taasisi zitaanza kutoka kwenye malengo yake ya kuanzishwa endapo zitalazimishwa kuwaza Gawio kila mwaka.

Badala ya kutoa elimu zitaanza kukomaa kutoza faini, kubana mambo ya kiofisi kama kuongeza uwezo kwa wafanyakazi n.k
 
Sijaona ttcl mwaka huu??? Vipi ATCL nayo, tuliambiwa Kuna ka faida kamepatikana mbona hawajatoa gawio???? Boss jana kasema kama hawana wauze hata magari yao ili mradi watoe gawio
 
NHC IMENISTAAJABISHA SANA KWA NINI MCHANGO WAO NI KIDUCHU MNO?,LAZIMA KUNA WALAKINI HAPO.SI BUREE .....!
 
Aloo hili swala lina hitaji ufafanuzi .Almost wakati mimi nafatilia kitambulisho huduma zilikuwa bure au sasa hivi kuna malipo.?
 
Yani sijaona ya kufikisha 5.2B , mmepika tu midata
 
IFM nayo imetoa gawio la 2 billion?

Dunia nzima Public University zinaendeshwa kwa ruzuku ya Serikal na zile Ada ni sehemu ndogo tu
Usikariri ndugu, vyuo vyote ambavyo viko chini ya Taasisi za Serikali ziliruhusiwa kujiendesha zenyewe kwa Faida tangu kipindi cha Mkwere kasoro vyuo vichache tu vinavyohudumiwa na Serikali kuu
 
Usikariri ndugu, vyuo vyote ambavyo viko chini ya Taasisi za Serikali ziliruhusiwa kujiendesha zenyewe kwa Faida tangu kipindi cha Mkwere kasoro vyuo vichache tu vinavyohudumiwa na Serikali kuu

Unajiendeshaje kwa Faida wakati wote Mishahara inalipwa direct kutokea utumishi/Hazina?

Au neno kujiendesha kwa faida hujui?
 
Nadhani wanakosea kuita gawio, makampuni kama Nida na TPA na mengine ya aina hiyo yanabanwa na finance act nadhani ya 2013 inayoyataka kutoa 15% ya gross income kwenda hazina
 
IFM ni chuo kilicho chini ya wizara ya fedha, kuna uwezekano mkubwa mishahara inalipwa na serikali hivyo huwa na ziada ya kutosha ya fedha za kupelek hazina
Kaangalie taarifa za fedha za ifm
 
Mfano ifm na udsm ikiwakilisha vyuo.......udsm tu 2017 ilipata ruzuku bilioni 78 toka serikalini ,ada bil 34 ,mishahara tu bil 80 ,bila ruzuku hawabaki na kitu.........gawio watoe wakati hawajitosherezi ?au tuite return tu
 
Attachments

  • Screenshot_20191126-001132.png
    43.1 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…