NIDA yakabidhi kiasi cha TZS 61,053,535,363 Serikalini kwa maendeleo ya Wananchi

NIDA yakabidhi kiasi cha TZS 61,053,535,363 Serikalini kwa maendeleo ya Wananchi

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
IMG-20260630-WA0095.jpg.jpeg
Dar es Salaam, 1 Julai 2026
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa tarehe 30 Juni 2026, imekabidhi Serikalini mchango wa TZS 61,053,535,363 ikiwa ni fedha za makusanyo yake katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamuhuriy a Muungano wa Tanzania ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mchango huo ulikabidhiwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hafla ya upokeaji wa gawio na michango ya Taasisi za Umma iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, NIDA pia ilipata heshima ya kutunukiwa tuzo baada ya kushika nafasi ya pili miongoni mwa Taasisi zilizofanya vizuri katika kuwasilisha mchango wake Serikalini. Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Mheshimiwa Rais, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa NIDA katika kuimarisha mapato ya Serikali na kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji amesema mafanikio hayo ni matokeo ya kuendelea kuimarishwa kwa mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi.
IMG-20260630-WA0097.jpg.jpeg
“Tunapokea heshima hii kwa unyenyekevu mkubwa. Mchango huu siyo tu takwimu za kifedha, bali ni matokeo ya uboreshaji wa huduma za utambuzi wa Taifa ambapo ni nyenzo muhimu katika kuimarisha usalama, kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kichocheo cha mapato katika sekta binafsi na Umma,” amesema Kaji.

NIDA inaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kusajili na kuwatambua wananchi kwa kutoa Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN) na Vitambulisho vya Taifa, pamoja na kuwezesha matumizi ya taarifa sahihi za utambuzi katika sekta mbalimbali za huduma za umma na binafsi.

Utambuzi wa Taifa ni msingi muhimu katika kuwezesha Serikali na Sekta Binafsi kupanga, kuhudumia wananchi au wateja wake kwa ufanisi, kuimarisha usalama, kudhibiti mianya ya udanganyifu na kuongeza tija katika utoaji wa huduma.

NIDA inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono, miongozo na uwekezaji unaoendelea kufanywa katika kuimarisha mifumo ya utambuzi nchini.

Aidha, NIDA inawashukuru wananchi, wadau, taasisi za Serikali na sekta binafsi kwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka katika kujenga Taifa lenye utambuzi sahihi, huduma bora na maendeleo jumuishi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati
 
Aisee! Wakati huo kuna baadhi ya Watanzania hawajapata Vitambulisho harafu wanarudisha fedha serikalini?
Na huenda sababu mojawapo wanayotoa ni ukosefu wa fedha!
Anyway sawa tu!
 
NIDA wanafanya biashara siku hizi, na kama wameweza kurudisha hizo je walipata ngapi kuna mengi sana hatujui, ngoja kukuchee
 
Kwahiyo wanauza taarifa zetu. Sheria ya taarifa binafsi zikoje? mkuu kuna kitu hakija kaa mkao
Kwenye sheria ya taarifa kuna sehemu mbili, producer and processor

NIDA ndio producer and mzalishaji mkubwa wa hizo data na ndio mmliki wake kisheria
 
Back
Top Bottom