Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
September 15 ni siku ya kimataifa ya demokrasia duniani ambapo nchi mbalimbali duniani hupata fursa ya kujadili demokrasia ya nchi zao na wadau husika wa demokrasia katika nchi hizo kama vile vyama vya upinzani.
Sasa sielewi mantiki ya Rais Samia Suluhu Hassan kuitumia hiyo siku ya leo kuzungumza na wanawake wa Tanzania (mara ya pili) na sio wadau wa demokrasia (vyama vya siasa).
Katika hali ya kawaida nilikuwa nategemea Rais akutane na wadau wa demokrasia kama vile vyama vya upinzani kisha wajadili hatima ya demokrasia ya nchi yetu lakini yeye anakutana na wanawake na tena hii ni mara ya pili.Kwangu mimi jambo hili haliingii akilini.
Au siku ya wanawake Duniani (March 08) ndiyo atakutana na wadau wa demokrasia (hususani vyama vya siasa) kujadili masuala ya kidemokrasia?
Sielewi mantiki ya kuwakimbia wapinzani wake wa kisiasa ambao ndiyo wadau wakubwa wa demokrasia hapa nchini.Nielewesheni
Ukiangalia picha ya pili hapo chini Tanzania tumezidi kushuka katika marks za demokrasia duniani ambapo sasa hivi tumeshuka kutoka marks 40/100 hadi kufika marks 34/100.
Yaani kama ni mtihani wa darasani maana yake ni kwamba umepata marks 34 kati ya mia.Hii si kupata F?
Hii maana yake ni kwamba bado kidogo tunaingia kwenye “not free countries” kwa sababu ya kuminya haki za kisiasa na za kiraia halafu Rais siku ya demokrasia duniani kama ya leo anaenda kukutana na wanawake badala ya kukutana na wadau wa demokrasia.