Nielewesheni; Magufuli alisema hatutafanya lockdown kwani nchi jirani zinategemea bandari zetu, nchi jirani zinazuia magari toka kwetu kuiingia kwao!

Nielewesheni; Magufuli alisema hatutafanya lockdown kwani nchi jirani zinategemea bandari zetu, nchi jirani zinazuia magari toka kwetu kuiingia kwao!

Makubwa haya! Lakini Zanzibar wameshasema uchaguzi utafanyika - sasa uchaguzi utafanyikaje Zanzibar na bara usifanyike?
Zanzibar wanajisemea tu lakini hawajui kilichopo kichwani mwa mtukufu malaika tokea chato ni kufuta uchaguzi mkuu
 
Ebu fikiria wenyeviti wa Serikali za mitaa wote ni wa CCM lakini cha ajabu hawahangaiki kuzuia wananchi wao kukaa vijiweni vibarazani kurundikana kuambukizana hovyo, wameamua watanzania wafe kiwepesi lakini sasa Duniani kote wamejua Tanzania inasaka kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mkuu kwa kuwatoa Raia wake kafara kwa njia hizo za kuruhusu umati vijiwe watu kujazana makanisani misikitini misibani na sasa tarehe 22 may 2020 watafungua shule watoto wakaambukizane mashuleni wafe na walimu wafe sababu kuu ni kusaka kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mkuu.
 
Lakini hata hivyo, ilikuwa muhimu sana kwa Tanzania kuwa na mkakati wa pamoja na hizi nchi ukizingatia kuna suala la bidhaa zao kupitia kwetu. Sasa ajabu hatuna mawasiliano ya hivyo hata Museveni kasema hivyo. Mkutano wa SADC raisi wetu kasusia!
... kwa maelezo yako hayo wakulaumiwa sio wao ni sisi ambao tunaonekana kutotoa ushirikiano na majirani dhidi ya gonjwa hili. Adui amevamia kijiji, la mgambo limelia wanakijiji wote isipokuwa wewe wamekusanyika wanamsaka "simba mla watu"; inagundulika "simba mla watu" huyu anaishi ndani kwako huku wewe umepiga kimya! Kama sio mchawi wakuiteje?
 
Makubwa haya! Lakini Zanzibar wameshasema uchaguzi utafanyika - sasa uchaguzi utafanyikaje Zanzibar na bara usifanyike?
Hujawahi kusikia Zanzibar ni nchi? au siyo nchi! hapo ndiyo wanapapenda!
 
Nilimshangaa sana Rais kwa maamuzi yake japo alinisusa!! na kuniita majina mabaya
 
Hujawahi kusikia Zanzibar ni nchi? au siyo nchi! hapo ndiyo wanapapenda!
... uchaguzi ni suala la muungano? Ule wa Rais wa JMT na wabunge ni suala la muungano ila ule wa Rais SMZ na wawakilishi sio suala la muungano. So, Zanzibar wanaweza kufanya huo wa pili bila kuhitaji "baraka" za muungano.
 
Wizara ya Elimu imejipanga kufungua shule lengo likiwa ni kwenda kuongeza maambukizi zaidi, WHO wanajua vituko vyote vinavyofanywa na Tanzania ndiyo maana wamewambia Nchi jirani wawakatae watanzania.
 
Ummoja ni nguvu,Bila ushirikiano tutakwama sababu ya ubishi.
Mambo ya kutunisha msuri bila kutunisha maarifa yameanza kutugharimu.

Uganda,Rwanda,Burundi, Zambia,Congo DRC ,Malawi,wana alternative routes.
 
Jipe muda utajua Tanzania ni nchi ya namna gani Zambia hawawez kufunga mipaka wameongea tu kwenye vyombo vya habari Basi Kama anavyo ongea Kenya et Ana Lock down wakati watu wanazurula tu mtaani
Mara nyingine nashindwa kuelewa kama mie ndio mwenye tatizo la kuelewa mabo au ni wale ninaowasikiliza wenye tatizo hilo.

Hap nyuma tuliambiwa kwamba hatutakuwa na lock down kwa ajili ya corona kwa kuwa nchi jirani zinatutegemea kuwafikishia bidhaa zao. Hata mifano ikatolewa ya Rwanda, Zambia, DRC na kdhalika.

Baada ya muda nikasikia kwenye mpaka wetu na Rwanda madereva wa malori toka Tanzania wanazuiwa kuingia nchini Rwanda kuwapelekea bidhaa zinazoingia kupitia bandari zetu. Na sasa nasikia Zmbia nao wamefung mpaka japo sisi tuko tayari kuwendelea kuwapelekea bidhaa zao zinazoptia hapa kwetu.

Hebu nielewesheni, kwa nini hawa jamaa wanafanya hivi wakati lengo letu ni kuwaonyesha roho yetu nzuri kwa majirani? Kwa nini hawatuelewi lakini? Hawaoni kwamba raisi wetu ana ufikirio sana kwao?
I

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hata hivyo, ilikuwa muhimu sana kwa Tanzania kuwa na mkakati wa pamoja na hizi nchi ukizingatia kuna suala la bidhaa zao kupitia kwetu. Sasa ajabu hatuna mawasiliano ya hivyo hata Museveni kasema hivyo. Mkutano wa SADC raisi wetu kasusia!
WHO wana taarifa zote juu ya vituko vya Serikali ya CCM isiyojali Afya za wananchi bali inaangalia jinsi ya kufaidi pesa iliyotengwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu pindi ukifutwa, sasa wanaangalia pesa badala ya uhai na Afya za watanzania
 
Jipe muda utajua Tanzania ni nchi ya namna gani Zambia hawawez kufunga mipaka wameongea tu kwenye vyombo vya habari Basi Kama anavyo ongea Kenya et Ana Lock down wakati watu wanazurula tu mtaaniI

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuingia kenya mpaka ukae siku 14 kenya wanapiga vita kweli hawataki mikusanyiko misikitini makanisani wala watu kukaa vijiweni kama hapo Tanzania kwetu
 
This is the point. Hauwezi kupigana na cross-border disease on your own. Lazima ufanyekazi na majirani. Maadam jirani ana COVID-19 na wewe utakuwa nayo tu.
Lakini hata hivyo, ilikuwa muhimu sana kwa Tanzania kuwa na mkakati wa pamoja na hizi nchi ukizingatia kuna suala la bidhaa zao kupitia kwetu. Sasa ajabu hatuna mawasiliano ya hivyo hata Museveni kasema hivyo. Mkutano wa SADC raisi wetu kasusia!
 
Hold on, wanazuia malori kuingia kwao au wanazuia na mizigo pia.?

Nikafikiri kuna utaratibu wa kupokea mizigo mpakani ili wa huku warudi na mizigo ipokelelewe na dereva mwingine, ooh kwa aliyeelewa anieleweshe hili likoje.
 
zambia hawafanyi cheap politics km bongo..watu huko wapo serious na maisha ya raia wao

Sent using Jamii Forums mobile app
Watalii hata corona ikipita hawatakuwa na imani na Tanzania baada ya kushuhudia wakificha taarifa za wagonjwa wa corona wakikazania kutangaza waliopona wakati waliopona wanaambukizwa tena kwa mara ya pili baada ya kwenda kushinda vijiweni Bar misikitini makanisani kwenye misongamano mikusanyiko mikubwa.
 
Kenya uganda wanazuia watanzania wanakaa siku 14 mipakani wanapimwa sana, watanzania wamesuswa na Nchi Jiran baada ya kuona wabunge waziri na viongozi wengi wamekufa kwa uzembe tu
Kwa hiyo huko kenya watu hawafi? Huko Uganda watu hawafi? Au bado unawazia ile kasima ya manispaa ya ubungo ambayo kuna watu wanaivizia?
 
Mra nyingine nashindwa kuelewa kama mie ndio mwenye tatizo la kuelewa mabo au ni wale ninaowasikiliza wenye tatizo hilo.

Hap nyuma tuliambiwa kwamba hatutakuwa na lock down kwa ajili ya corona kwa kuwa nchi jirani zinatutegemea kuwafikishia bidhaa zao. Hata mifano ikatolewa ya Rwanda, Zambia, DRC na kdhalika. Baada ya muda nikasikia kwenye mpaka wetu na Rwanda madereva wa malori toka Tanzania wanazuiwa kuingia nchini Rwanda kuwapelekea bidhaa zinazoingia kupitia bandari zetu. Na sasa nasikia Zmbia nao wamefung mpaka japo sisi tuko tayari kuwendelea kuwapelekea bidhaa zao zinazoptia hapa kwetu.

Hebu nielewesheni, kwa nini hawa jamaa wanafanya hivi wakati lengo letu ni kuwaonyesha roho yetu nzuri kwa majirani? Kwa nini hawatuelewi lakini? Hawaoni kwamba raisi wetu ana ufikirio sana kwao?
Ukitaka kuelewa jinsi ulimwengu ulivyo naomba sikiliza hii Audio:

Katika Afrika nchi ambayo iko independent na ambayo inaubavu wa kuweza amua mambo yake yenyewe ni Tanzania tu mdogo wangu. Nchi zote nyingine za Afrika zimekuwa hijacked na mabeberu. Believe me! Usiwe suke na mazuri ya vitani wako. Huo ni moto ambao umefunikwa na majivu mengi.

Kenya, Uganda na Rwanda hawako sawa na sisi. Marais wa nchi hizi zote ni Mapappett tu wa wazungu. Umeona hivi juzi juzi Rais Kenyatta alivyo jikomba kwa wazungu? Subiri nitaku-update na data.

Na isitoshe Rais Magufuli aliomba IMF na World Bank wasamehe baadhi ya madeni yao kwenye kipindi hiki cha janga la Coronavirus ili hizo nchi ziweze pambana ma hili janga, umesikia hizo nchi zilicho fanya? Faster faster wamekubali kupokea mikopo kipya kutoka hao mabeberu. Huu sasa utauhitaje? Sio unafiki huo?

Hao ndiyo Marais tunao taka kuwa nao kwenye East African Community

Sisi tuna bahati ya lugha yetu ya kiswahili. Kiswahili ni lugha ya amani. Wazungu wamejaribu sana kutufarakanisha wameshindwa. Ndiyo maana wanatuletea Stations zao BBC, VOA na DW katika lugha yetu ili waweze kutumanipulate.

Kenya inatumiwa sana na wazungu kutuvuruga sisi. Toka enzi ya Nyerere.

Wahenga watakumbuka Vita vya Kagera mkenya ambaye tuna damu moja alitusaliti sisi na kumsaidia Idi Amini Dada.

Fumbua macho ndugu yangu. Usipende ya wazungu na majirani ukafiri utakuwa salama.

Rais Magufuli amewashtukia sasa. Imechukua mda mrefu sana. Nafikiri sasa ameanza kuelewa kuwa sisi tuko peke yetu.

Wewe nchi ambayo inapoteza Uhuru wake na kuwaacha wazungu waje kusuruhisha mgogoro wao unategemea kushirikiana nao?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kuelewa jinsi ulimwengu ulivyo naomba sikiliza hii Audio:
Conspiracy theories.

Hakun hata chembe ya ushahidi katika hiyo recording. NI maneno tu ya mtu ambae bila shaka ni shabiki mkubwa wa Magufuli, au wale watu ambao wako kwenye "dola" iliyoko madarakani ambao lazima wataitetea. Kwa hiyo siwezi kuchukulia yanayosemwa kuwa ukweli ulivyo
 
Back
Top Bottom