Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

Root root AE

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
207
Reaction score
354
Wakuu heshima zenu.
Moja kwa moja kwenye mada husika.

Nataka kwenda South Africa kujaribu bahati yangu huko pia,maana uwanja wa nyumbani naona maji yananizidi kina kila uchwao...simaanishi kwamba nimejaribu kila kitu hapa nyumbani bongo "hapana" ,ila kuna baadhi ya vitu ambavyo huwa wanaume tunavifanya pale tunapokuwa desperate kuelekea the point of hitting-the-rock-bottom kwaajili ya kupata chochote kitu...sasa kusema ule ukweli siwezi kuvifanya hapa nyumbani(na hii ni kwasababu zangu binafsi ambazo kwako huenda ukaona ni sababu za kipuuzi,ila utofauti huu wa kimtazamo ndio sifa moja ya binadamu kamili right?)....

Sasa baadhi ya vitu ambavyo nipo tayari kuvifanya nje na sio hapa nyumbani ni kama kubeba mizigo bandarini/viwandani,kuuza vitu kwenye traffic jam,kutembeza bidhaa kitaa(street vendoring),....nk nahisi ushapata picha nini namaanisha.
Sasa kati ya nchi zote nimeichagua south africa sababu ya diversity ya hustlers waliopo kule, sasa shida ni kwamba siyajui kiundani majiji haya matatu Capetown, Pretoria na Johannesburg.

Hivo kwa mwenye kujua au anayeishi katika moja ya majiji hayo naomba kujuzwa taarifa za msingi kuhusu majiji haya matatu.
Asante.

"We're born to suffer"
Lucky Dube
 
Kama umeshindwa hustle nyumbani ukiwa free kabisaa sidhani kama huko south.A kuna kipya zaidi ya mateso, ubaharia ni jina tuu ila kiukweli hakuna kipya zaidi ya majuto na kuteseka else uwe na kitu cha msingi kinachokupeleka...mark my words!
Umewahi kwenda?umewahi kuishi? Au unarudia ulichokiskia tu pasipo ushahidi...
Isitoshe mimi sio baharia naenda kwa njia official kabisa
 
Hapa hapa kwa nyerere,ya nini niende ulaya,sijui hata misele ya huko,kuishi kama dikidiki kwenye msitu wa simba mimi siwezi, zamani palikuwa panaishu huko sio sasa hivi binadamu wametengeneza roho mbaya,nisije bure nikatolewa bandana na Figo yangu,ugali wa mlenda na daga wa mwanza nitawapati wapi nikienda huko,daah eti nikabebe maboks,mara town kuuza vinywaji kwenye magari mmhhh nani anataka maisha ya kiwaki hivyoo,naseti mipango na toboa hapa hapa bongo,mbona wazazi wangu wamenilea vinzuri bila ya kwenda South??hauna ndugu wala jamaa sindo unaenda kuwa bwabwa 🤭🤭🤭
 
Mbona povu limekutoka ivo mkuu??
Kwani anayeenda ni wewe au mimi...bongo hapa hapa kuna watu wanaishi kama mbwa na nchi yao...ni kubadilisha mazingira tu lakini tukiongelea swali la mtindo wa maisha kiujumla hakuna jipya linalofanyika nchi nyingine afu bongo halipo....
 
Back
Top Bottom