Hizi mada zinakuja sana humu JF,na wengi wanaochangia ni watanzania waliojaa husuda, fitina, kukatishana tamaa na kebehi nyingi tu, mtoa hoja sikiliza mkuu maisha ni popote hapa duniani, kufa tunakufa popote usiogope, jiandae kisaikolojia kichwani na uelewe na uamue kuwa no turning back, good luck mkuu nenda kajaribu maisha, kule kuna dudula hapa kuna panya road usiogope, ukifika wabongo kaa nao mbali sana, wengi wako kama hawa humu wanaokukatisha tamaa, jhb ni kama Dar, pilika nyingi, mzunguko wa pesa upo, kifo kipo mkononi ila ndio sehemu ya kutafuta, Durban kuna opportunities nyingi sana hasa za ujenzi baada ya yale machafuko ya July, Capetown ni mji mzuri mno ila kwa waliojijenga tayari, kuko peace ila cost of living ipo hai, kwangu kama umekomaa kichwani ingia jhb straight, again kiswahili cha kibongo wakimbie, jichanganye na warundi,wakongo, wakenya even wapopo, good luck mkuu,ukifanikiwa on the way back via lingusenguse tusalimiane