Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

Tafuta chuo huko chenye course ya 3 yrs apply, ukikubaliwa andaa hela ya bima ya afya ya mwanafunzi hii inalipiwa mwaka mmoja, baada ya hivi vitu ukiwa na passport nenda ubalozini kwao ndani ya mwezi mmoja permit iko tayar kwa wewe kwenda zako huko, hii njia ni bora ambayo nita m recommend mtu yeyote anayetaka kwenda south kuitumia

Kwasababu gani 3, wakati ukiwa huko permit yako itakupa muda mrefu wakutafuta kazi... Kila la kheri
Asante, hivyo hiyo bima ni kiasi gani? Pia kwa ujumla niandae bajeti ya kiasi gani itakayo niwezesha kuishi huko kabla sijapata kazi? Nisaidie kunielewesha maana mimi ni miongoni mwa watu tunaotafuta namna ya kujinasua
 
Asante, hivyo hiyo bima ni kiasi gani? Pia kwa ujumla niandae bajeti ya kiasi gani itakayo niwezesha kuishi huko kabla sijapata kazi? Nisaidie kunielewesha maana mimi ni miongoni mwa watu tunaotafuta namna ya kujinasua
Huku kama unayo mtu wakukupokea hapo kakupunguzia mzigo kwenye chakula na malazi, maana wakati wakutafuta ukiwa na makazi na chakula, akili inakuwa inatulia kwenye kutafuta kazi tuu.... Bima zipo za namna nyingi yani ni kama classes za maisha kuna first, middle na classes ya mwisho. Sasa wewe mfuko wako unaegemea class gani hapo,kwenye kutaka bima?
 
mbona kawaida tu, mbona kuna wa america (Mexican, Cuban,) wanazamia america ,usa .
Kuna wazungu kibao wa western europe wanazamia tu nchi nyingine za ulaya mashariki?
hata hujaelewa somo. usifananishe western europe, america ya kaskazini na huo uswahili. America is America, Europe is Europe, and Africa is AFrica.
 
Wakuu heshima zenu.
Moja kwa moja kwenye mada husika.

Nataka kwenda South Africa kujaribu bahati yangu huko pia,maana uwanja wa nyumbani naona maji yananizidi kina kila uchwao...simaanishi kwamba nimejaribu kila kitu hapa nyumbani bongo "hapana" ,ila kuna baadhi ya vitu ambavyo huwa wanaume tunavifanya pale tunapokuwa desperate kuelekea the point of hitting-the-rock-bottom kwaajili ya kupata chochote kitu...sasa kusema ule ukweli siwezi kuvifanya hapa nyumbani(na hii ni kwasababu zangu binafsi ambazo kwako huenda ukaona ni sababu za kipuuzi,ila utofauti huu wa kimtazamo ndio sifa moja ya binadamu kamili right?)....

Sasa baadhi ya vitu ambavyo nipo tayari kuvifanya nje na sio hapa nyumbani ni kama kubeba mizigo bandarini/viwandani,kuuza vitu kwenye traffic jam,kutembeza bidhaa kitaa(street vendoring),....nk nahisi ushapata picha nini namaanisha.
Sasa kati ya nchi zote nimeichagua south africa sababu ya diversity ya hustlers waliopo kule, sasa shida ni kwamba siyajui kiundani majiji haya matatu Capetown, Pretoria na Johannesburg.

Hivo kwa mwenye kujua au anayeishi katika moja ya majiji hayo naomba kujuzwa taarifa za msingi kuhusu majiji haya matatu.
Asante.

"We're born to suffer"
Lucky Dube
fungua duka la vyakula na bidhaa mchanganyiko kama la Mangi. Utanishukuru baadaye. south Africa ndiyo chimbuko la shida kwa africa. utakuja kujuta
 
Nenda miji mdogo kama Kimberley au Gqeberha. Ishi locations (kwenye slums) fungua saloon
 
Back
Top Bottom