Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

tafuta nchi ya ulaya nenda kazamie huko, africa hata ukienda jobagi au takataka gani mii yote ni shit hole tu. mwafrika unazamia africa? wapi na wapi?
 
Kama mbongo mwenzangu naomba nikushauri mambo machache.

1. Passport
Hakikisha wakati unakuja huku angalau passport yako iwe badobado mpya, toka umeipata mpaka sasa. Kwaana gani unapokuja huku unakuja kutafuta maisha so inamaana mpaka michongo ikae vizur itakuchukua kipindi kidogo ili usije ukapata usumbufu, umepata kazi then passport ndio inaishia muda wake

2.Visa.. Njooo na viza inayoelewa kwa maana ya visa yako ya kukaa huku iwe angalau sii chini ya 3 yrs, kwanini nasema hivi 3 ukiwa huku tayari umepata mchongo na saving ushaweka so unawaza tena kuja bongo na ku renew viza yako then unarudi...
 
Kwanini mara nyingi mnasisitiza wanaoenda ughaibuni wakae mbali na wabongo wa huko ?
 
Nenda NAMTUMBO maana hao unawafuata huko wanapatikana Namtumbo
 
Kijana anakaa S.Africa mika 20 akifa kumsafirisha inakua issue wanazika hukohuko.
kwao njaa wanauliza kaacha nini mtutumie,wanaambiwa akuna sasa unajiuliza si angebaki home akawasaidia wazazi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu samahani, hiyo visa ya 3 years unaipataje?
 
tafuta nchi ya ulaya nenda kazamie huko, africa hata ukienda jobagi au takataka gani mii yote ni shit hole tu. mwafrika unazamia africa? wapi na wapi?
mbona kawaida tu, mbona kuna wa america (Mexican, Cuban,) wanazamia america ,usa .
Kuna wazungu kibao wa western europe wanazamia tu nchi nyingine za ulaya mashariki?
 
Namba 3 upo sahihi??
 
Kwa ujumla kaka ungeamua mwenyewe tu na moyo wako ni mji gani ukadondokee pale kaburu ila ukisema ufuate ushauri wa wabongo nakwambia hatutoboi hata kidogo. Sisi wabongo kazi yetu ni kutishana na kuvunjana moyo tu.... Mi nakushauri usiku wa Leo kaa na halmashauri yako ya kichwa then hasubuhi utoke na majibu wewe kama wewe then yafanyie kazi.
 
Kwanza elewa kwamba wanaokukosoa kabla hujaondoka ni wazuri sana kwako, kuliko wanaokuunga mkono kabla hayajakupata!
Siku zote mwenye akili atachukua tahadhari ambayo ni nzuri mno kimafanikio.
Pili, ni kweli hata hapa bongo unaweza kufanikiwa kwa juhudi ileile utakayofanya kule Bondeni ufanikiwe.
Tatu, wakati wa sasa kazi za kibishi kila mahali zimekabwa!
Zamani ilikuwa uhakika zaidi.
Siku hizi kuzamia ni sawa na kucheza bonanza la mchina
 
Tafuta chuo huko chenye course ya 3 yrs apply, ukikubaliwa andaa hela ya bima ya afya ya mwanafunzi hii inalipiwa mwaka mmoja, baada ya hivi vitu ukiwa na passport nenda ubalozini kwao ndani ya mwezi mmoja permit iko tayar kwa wewe kwenda zako huko, hii njia ni bora ambayo nita m recommend mtu yeyote anayetaka kwenda south kuitumia

Kwasababu gani 3, wakati ukiwa huko permit yako itakupa muda mrefu wakutafuta kazi... Kila la kheri
Mkuu samahani, hiyo visa ya 3 years unaipataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…