Udochi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 787
- 1,056
Umepata kwa Sh. ngapi mkuu?Namshukuru Mungu nimepata bati za Alaf na kazi inaendelea. Asanteni kwa ushauri wenu
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umepata kwa Sh. ngapi mkuu?Namshukuru Mungu nimepata bati za Alaf na kazi inaendelea. Asanteni kwa ushauri wenu
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Shida ya hizi kampuni mpya tena za kichina. Unashangaa bati linapauka kabla hata hujahamia
Karibu paalako co.ltd kwa bati imara na bei nafuuMm Niko njia panda naambiwa bati za Alaf ndio bora sana nataka nipaue ila bei ya alaf ipo juu sasa sijui nivute subra niongezee hela ili ninue alafu ,maana naambia mengine yanapauka
Kampuni za uswahiliKaribu paalako co.ltd kwa bati imara na bei nafuu
Warranty 10 years bila kupauka au kupata kutu
Nicheki kwa mawasiliano zaidi nikupe bati Bora kwa bei ya kiwandani 0755732369
Unataka kumliza mtu na vipesa vyake vya kuungaunga. Hauna huruma mkuuKaribu paalako co.ltd kwa bati imara na bei nafuu
Warranty 10 years bila kupauka au kupata kutu
Nicheki kwa mawasiliano zaidi nikupe bati Bora kwa bei ya kiwandani 0755732369
We jamaa unakijua unachoongea?? Fatilia uzi humu unaenda kwa Heading" Elimu kuhusu Mabati"Nenda na Alaf.
Sunshare na kiboko ni takataka
Ndio hizo hizoKampuni za uswahili
Watu wengi hawana elimu kuhusu Mabati. Nashauri watafute uzi humu wa Elimu kuhusu Mabati.Nenda kachukue sunshare.Kwanza wana vipimo vya huakika wanapima uber sawa rangi na uimara wa bati.Alaf ni jina tu lakini bati zao ni za kawaida sana.kachukue gauge 30 pale sunshare huto juta.
Naomba nitoe mchango wangu kutokana na nilichojifunza kwa muda mfupi kwenye hii industry ya roofing.Nenda na Alaf.
Sunshare na kiboko ni takataka
Huu ni uchunguzi wangu binafsi niliofanya baada ya kukutana na contradicting stories nyingi mtaani. Nikaja na hizo findingsNaomba nitoe mchango wangu kutokana na nilichojifunza kwa muda mfupi kwenye hii industry ya roofing.
Kwanza nisema watu wengi kila siku wanajenga au kufanya biashara hizi lakini kuna mahali wanafeli ku grasp taarifa sahihi za kitaalam.
Nitazungumzia viwanda nilivyotembelea Alaf, Sunshare, Bati Bomba na kingine pale Tabata..
Gauge za mabati hutofautiana kulingana na unene au thickness ya bati, G30 inakadiriwa kuwa na thickness ya 0.25mm na G28 ni 0.35mm. This is techinical diferences. Na pia kuna chemical diferences lakini karibu zote zinafanana maana zimeundwa na Aluminium na Zinc ktk ratio tofauti tofauti. Zinc na Aluminium ndio properties zinazozui bati kuota kutu kama ikiform zinc oxide au Aluminium Oxide.
Matumizi ya Gauge ktk nyumba.
Kama mleta mada alivyouliza nini tofauti ya matumizi ya bati G28 dhidi ya G30.
1. Hutegemea na mahitaji ya mjengaji, mfano serikali inayojenga majengo makubwa kama kiwanda, godauni, shule au hospitali hutumia bati zenye thickness kubwa kutokana na umuhimu wa jengo lenyewe tofauti na mtu binafsi anayejenga nyumba ya vyumba vitatu.
2. Uimara wa nyumba, msingi na teknolojia ya ujenzi. Hapa tunaona kuwa nyumba kubwa inahitaji mabati mengi zaidi. Lakini pia kama nyumba imejengwa na Fundi Maico yatarajiwa viwango vyake vya uimara( strength) ya msingi na ukuta vitakuwa si mujarabu hivyo kuezeka nyumba hii kwa G28 inaweza kupeleka uzito mkubwa unaoweza kuhatarisha maisha ya nyumba yako. Vile vile kama hali ya hewa ya udongo, maji kutwama, mmomonyoko n.k vyaweza kupelekea nyumba kutitia.
Hii ni muhimu kwa sababu Bando la bati 16 , G28 lina karibu uzito wa kilo 92 wakati bando la bati 16 G30 lina uzito wa takribani kilo 50. Kwahiyo nyumba kubwa kama shule, godauni, kanisa au hospitali utajenga kwa bando ngapi na huo msingi na ardhi vitahimili hizo tani za uzito wa paa??
3. Teknolojia ya uezekaji. Hii inaenda sambamba na ukubwa wa jengo. Nyumba zetu hizi kenchi hadi kenchi ni mita moja tu au chini ya hapo. Shule na kanisa au msikiti vipimo ni vikubwa zaidi so yafaa G28.
Kuhusu Bei za Mabati kutofautiana.
Katika uchunguzi wangu nilifikia hitimisho kuwa hakuna tofauti kubwa ktk bei na utofauti wa bei haumanishi yenye bei kubwa ni imara na bora zaidi. Fuatana nami:
Wauzaji wengi watakueleza kuhusu Gauge ya bati, rangi, na urefu na bei kamwe hawakwambii upana wa bati.
Mfano. Kiwanda cha tabata bati la G30. Migongo mipana( msauzi) urefu futi 10 linauzwa elfu 30. Bati hilo hilo Kiwanda cha Bati Bomba wanauza elfu 28,500. Lakini ni hivi upana kwa Tabata ni 750mm wakati BatiBomba ni 90mm. Vivyo hivyo Sunshare bati zao upana ni 870mm na wanauza elfu 34,500 kwa bati hilo hilo la urefu futi 10, G30 na rangi ile ile.
Kwa G28 Batibomba wanauza futi 10 migongo mipana kwa 34500 wakati ALAF wanauza takriban 55,500. Unaweza kudhani Alaf wanauza bei kubwa sana lakini ALAF bati zao upana ni 1220mm wakati Batibomba ni 900mm. Hapa utaona kuna tofauti kubwa sana. Uki converge hizi factors kwa pamoja utakuta wote bei karibu sawa.
Mfano huo huo unaenda kwa Sunshare na Tabata.
So utahitaji kununua mabati machache ALAF a utahitaji mabati mengi Sunshare.
Jambo lingine linaloweza kuchangia utofauti wa Bei( usihusishwe na ubora au uimara) ni miundo mbinu ya uzalishaji mali pamoja na rasilimali watu.
Mfano. ALAF wana majengo mazuri ya kisasa ya kibiashara full kiyoyozi na ukifika pale kama uko nyumbani au ofisi ya CAG Kichere. Wakati ukifika Tabata na Batibomba joto na vumbi mwendo mdundo wanazalisha kwenye magodown hapo hapo ndio wateja wanachukulia mizigo yao. Hawa watu hawawezi kuchaji bei sawa. Lazima bei za pango na mandhari mazuri uyalipie. Hivyo hivyo kwa Makampuni mengine.
Ushindani wa kibiashara: makampuni mengine nje ya ALAF ni mapya na mageni. Hivyo wanaunafuu kidogo kutokana na mahitaji ya kujitangaza na kujitanua. ALAF tayari ni mkongwe wajenzi wa viwanda na serikali inachukua mizigo mikubwa kwake. Hana shida na hizo milioni zako 2,3, 4, 5...
Kuhusu Malighafi
Wote wananunua kwa supplier wanaofanana. Aidha South afrika au China na india. Na wote mali zao huingizwa zikiwa tayari zimeshachanganywa materials na Rangi. Kazi yao hapa Dar ni kukata na kukunja muundo unaotaka IT4, IT5, Versatile, Romantile....etc.
NB: mimi sio Injinia wa ujenzi wala sina any formal profession kwenye industry hii. Hii ni kutokana na elimu ya hapa na pale niliyodanya mimi mwenyewe kwa kuona, kuuliza, kushika na kusikia viwandani.
Penye makosa/ mapungufu wataalam karubuni kurekebisha.
Mfano. ALAF wana majengo mazuri ya kisasa ya kibiashara full kiyoyozi na ukifika pale kama uko nyumbani au ofisi ya CAG Kichere. Wakati ukifika Tabata na Batibomba joto na vumbi mwendo mdundo wanazalisha kwenye magodown hapo hapo ndio wateja wanachukulia mizigo yao.
Ni kweli na Bei za Alaf sio equivalent to Quality. Factors ni nyingi kama nilivyoeleza hapo.Alaf iko commited kwenye uzalishaji, ukiachana na upande wa marketing
milling sections zao ni kubwa kieneo , wana mitambo mingi na ya kisasa,
wana sections na sub-sections nyingi toka 'coil' linapoingia kwenye 'rolling mill' mpaka linapotokea kwenye 'forming mill' so final product lazime iwe yenye ubora, sio kanjanja
nenda kapige 'survey' ya kimtindo mle ndani then ulete mrejesho hapa
Endelea kuvumilia.Nimeagiza bati Alaf hadi Leo sijapata toka tarehe 9/2 mvua zimeanza nahisi kuchanganyikiwa. Sijui nifanyeje
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Ujuaji uwe na mipaka mzeeUnataka kumliza mtu na vipesa vyake vya kuungaunga. Hauna huruma mkuu
Ukikaribia jenga nishtue mkuuKampuni za uswahili
Acha ubabaishaji huwezi kupiga mtu humu bwana mdogoUjuaji uwe na mipaka mzee
Karibu nikuhudumie kwa bidhaa nzuri na bei nafuu karibu
Kutoka Buguruni kwenye hizo ofisi zao wanaweza kukufikishia mzigo Kibaha?Ukienda kwa wakala wao pale Buguruni karibu na ofisi za Azam utauzuwa ALAF og
Hii ni muhimu kwa sababu Bando la bati 16 , G28 lina karibu uzito wa kilo 92 wakati bando la bati 16 G30 lina uzito wa takribani kilo 50. Kwahiyo nyumba kubwa kama shule, godauni, kanisa au hospitali utajenga kwa bando ngapi na huo msingi na ardhi vitahimili hizo tani za uzito wa paa??
.
NB: mimi sio Injinia wa ujenzi wala sina any formal profession kwenye industry hii. Hii ni kutokana na elimu ya hapa na pale niliyodanya mimi mwenyewe kwa kuona, kuuliza, kushika na kusikia viwandani.
Penye makosa/ mapungufu wataalam karubuni kurekebisha.
Nashukuru kwa kuongezea nyama. lakini mfano uliotoa sio sawa na kile nilichoeleza. Nimesema unenzi wa nyumba zetu hizi za kiswahili. Wewe unazungmzia nyumba kubena uzito wa Slab ambayo ni level ya ghorofa hiyoina msingi wake heavy. Hizi za kwetu za vyumba viwili na sebure ni tofauti.Kwa sababu umesema wewe sio injinia basi acha nikufundishe..
Kwanza hii hoja ya uzito wa paa kwamba msingi utashindwa himili ni hoja mfu na ya upotodhaji!
Hivi nikuulize uzito wa zege la spab, beam, colums plus tofali na uzito wa bati kipi kizito? Kama msingi unahimili uzito wa slab na beams utashinwa himili kauzito ka bati?
Jua kwamba kabla ujenzi haujaanza usanifu lazima ufanyike na injinia. Na katika hatua hii ndio ana take into account na huo uzito wa bati unao usemea... Na huwezi jenga kabla ya usanifu haujafanywa na kupitishwa!
Unless uwe umetumia makanjanja mtaani ila mpaka msingi unajengwa jua washajua una uwezo wa kuhimili uzito wa bati na slab na kila kitu!
So hiyo hoja ya bati kuwa zito futa maana haina mantiki!
Sijajua mkuuKutoka Buguruni kwenye hizo ofisi zao wanaweza kukufikishia mzigo Kibaha?