Niezeke bati la kiwanda gani kati ya Alaf na Sunshare?

najua ALAF na SUNSHARE hazipauki lakini siwezi nunua bati moja elfu 40 ni bora hiyo pesa nifanyie finishing ya maana ndani.
Itunze hiyo hela utakuja kupakia rangi bati lako litakapopauka au kununua bati jipya baada ya paa kupauka ndani ya mwaka[emoji17]
 
Naomba msaada wenu kati ya bati za Alaf na Sunshare ipi bora. Fundi ananishauri nitumie Sunshare ila mimi napenda Alaf.

Bati moto ni za kampuni ya kichina inaitwa Dragon! Wana mabati safi sana sana! Kampuni hii in branches zake Mbeya, Makamako, Dar, na baadhi ya mikoa! Ni mabati mazuri sana Dragon! Au nimesema uongo ndugu zangu!
 
Nimeshazijua hizo nyumba za mabati yasiyoonekana. Zipo kama misikiti!
 
Ningeonapo kapicha ka nyumba iliyopauliwa kwa mtindo huo ningeweza kuhamasika zaidi,nina nyumba ya kupaua nakusanya nguvu

Zipo kama misikiti muundo wake! Bati safi ni za kampuni ya Dragon, kampuni ya kichina!
 
Nenda na Alaf.

Sunshare na kiboko ni takataka
Sikweli,Sunshare wanabati nzuri pia,japo Kwa Tz Alaf ndiyo inaongoza japo ukiezeka na Sunshare ni bati nzuri pia maana nina marafiki zangu wawili niliwachukulia pale Tazara mwaka wa 5 saizi,juni nimepita pale Mafinga bati bado inawaka
 
Nimeshazijua hizo nyumba za mabati yasiyoonekana. Zipo kama misikiti!
Inawezekana lakini naona misikiti huwa na minara.

.Kwa ujenzi wetu hatutumii kabisa bati. inakua ni "flat concrete roof" kwa kutumia vifaa maalum tunavyoviunda kwenye kiwanda chetu kidogo, ambavyo vinapubguza sana gharama ya ujenzi.

Picha baadae kidogo👇🏿

Your browser is not able to display this video.
 
Tafadhali tutembelee na sisi uje kujionea vifaa vyetu vya kuezekea na ujenzi wake. Ni tofauti na hao wote uliowatembelea. Tunajivunia ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.

Karibu sana, namba zangu ni 0625249605.
 
Bati moto ni za kampuni ya kichina inaitwa Dragon! Wana mabati safi sana sana! Kampuni hii in branches zake Mbeya, Makamako, Dar, na baadhi ya mikoa! Ni mabati mazuri sana Dragon! Au nimesema uongo ndugu zangu!
Unora kiaje sio kuja na maelezo ya jumla jumla tuu.
 
Tafadhali tutembelee na sisi uje kujionea vifaa vyetu vya kuezekea na ujenzi wake. Ni tofauti na hao wote uliowatembelea. Tunajivunia ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.

Karibu sana, namba zangu ni 0625249605.
Sawa mkuu Abdul nitakuja hapo baadae nadhani by August tutawasiliana.
 
Bati moto ni za kampuni ya kichina inaitwa Dragon! Wana mabati safi sana sana! Kampuni hii in branches zake Mbeya, Makamako, Dar, na baadhi ya mikoa! Ni mabati mazuri sana Dragon! Au nimesema uongo ndugu zangu!
Nilichukua mzigo Dragon mwaka jana. Nitaendelea kuwa shahidi mwaminifu kutia ushuhuda. Kuna watu walinitisha eti baada ya miezi sita zitachuja. Bado ni mpyaaa
 
Ukichukua bati kiwandani ALAF hakikisha unafanya escort mwenyewe mpaka site na wakati wa kupaua uwe hapo hapo ukikwepesha macho kidogo tu watu wanaingia nayo buguruni wanabadilisha faster unakua umepigwa
Acha kutisha watu bati sio dhahabu kiasi hicho
 
Muonekano wa kuezeka kwa vifaa vyetu ni huu...

View attachment 2259919
Na kwa ndani ni muonekano huu👇🏿

Hapo umepunguza gharama za mbao za kuezekea, umepunguza gharama za mabati, umepunguza msongamano wa mafundi, umepunguza gharama za mbao za kupigia gysum boards, umepunguza gharama za gysum boards, umeokoa nafasi kubwa ya kipaa. Na kama ulianza kujenga kwa msingi mzuri na ukajenga kuta kwa tofari zenye uimara unaokubalika, unakua umeshapata kiwanja kingine (ghorofa) juu ya nyumba yako.

Abraar Bricks Nyumba kwa Wote. Ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0625249605.
 
Endelea kufafanua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…