Asante kwa kufollow somo hiliBro should i have your number tafadhali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa kufollow somo hiliBro should i have your number tafadhali
Itunze hiyo hela utakuja kupakia rangi bati lako litakapopauka au kununua bati jipya baada ya paa kupauka ndani ya mwaka[emoji17]najua ALAF na SUNSHARE hazipauki lakini siwezi nunua bati moja elfu 40 ni bora hiyo pesa nifanyie finishing ya maana ndani.
Naomba msaada wenu kati ya bati za Alaf na Sunshare ipi bora. Fundi ananishauri nitumie Sunshare ila mimi napenda Alaf.
Hajafanya vibaya kukuelekeza kwetu. Tupo hapa JF na namba alizokupa ni zangu binafsi.
Nadhani Umewahi kusikia kuwa siku hizi Tanzania watu wanaezeka kwa mtindo ambao bati halionekani. Sisi tumeenda mbali na kisasa zaidi ya bati kutoonekana. Tunaunda (precast) vifaa maalum vya zege kwenye kiwanda chetu kidogo hapa Misugusugu, Kibaha. Pia tuna uwezo wa kuundà vifaa hivyo site ya mteja ili kupunguza gharama za usafirishaji vifaa.
Vifaa hivyo (slabs) vinakua mbadala wa bati na mbadala wa gypsum boards kwa pamoja.
Kwa vifaa hivyo Unapunguza gharama za kuezeka kwa bati, zinapunguza gharama za.mbao za bati, zinapunguza gharama za gypsum boards na mbao zake. Pia utapata nafasi juu ya kufanya chochote upendacho. Tuna supply vifaa na pia tuna mafundi wazoefu.
Programme yetu inaitwa Abraar Bricks Nyumba kwa wote. Ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa whatsqpp 0625249605.
Pia tunaweza kukujibu hapa swali lolote ulilonalo.
Karibu sana.
Ningeonapo kapicha ka nyumba iliyopauliwa kwa mtindo huo ningeweza kuhamasika zaidi,nina nyumba ya kupaua nakusanya nguvu
Duu alaf wameshapandisha bei baada ya mafuta kupanda
Na mimi nataka huo muda uwe kwenye maandishi
weka photo hilo paa
Sikweli,Sunshare wanabati nzuri pia,japo Kwa Tz Alaf ndiyo inaongoza japo ukiezeka na Sunshare ni bati nzuri pia maana nina marafiki zangu wawili niliwachukulia pale Tazara mwaka wa 5 saizi,juni nimepita pale Mafinga bati bado inawakaNenda na Alaf.
Sunshare na kiboko ni takataka
Inawezekana lakini naona misikiti huwa na minara.Nimeshazijua hizo nyumba za mabati yasiyoonekana. Zipo kama misikiti!
Tafadhali tutembelee na sisi uje kujionea vifaa vyetu vya kuezekea na ujenzi wake. Ni tofauti na hao wote uliowatembelea. Tunajivunia ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.Naomba nitoe mchango wangu kutokana na nilichojifunza kwa muda mfupi kwenye hii industry ya roofing.
Kwanza nisema watu wengi kila siku wanajenga au kufanya biashara hizi lakini kuna mahali wanafeli ku grasp taarifa sahihi za kitaalam.
Nitazungumzia viwanda nilivyotembelea Alaf, Sunshare, Bati Bomba na kingine pale Tabata..
Gauge za mabati hutofautiana kulingana na unene au thickness ya bati, G30 inakadiriwa kuwa na thickness ya 0.25mm na G28 ni 0.35mm. This is techinical diferences. Na pia kuna chemical diferences lakini karibu zote zinafanana maana zimeundwa na Aluminium na Zinc ktk ratio tofauti tofauti. Zinc na Aluminium ndio properties zinazozui bati kuota kutu kama ikiform zinc oxide au Aluminium Oxide.
Matumizi ya Gauge ktk nyumba.
Kama mleta mada alivyouliza nini tofauti ya matumizi ya bati G28 dhidi ya G30.
1. Hutegemea na mahitaji ya mjengaji, mfano serikali inayojenga majengo makubwa kama kiwanda, godauni, shule au hospitali hutumia bati zenye thickness kubwa kutokana na umuhimu wa jengo lenyewe tofauti na mtu binafsi anayejenga nyumba ya vyumba vitatu.
2. Uimara wa nyumba, msingi na teknolojia ya ujenzi. Hapa tunaona kuwa nyumba kubwa inahitaji mabati mengi zaidi. Lakini pia kama nyumba imejengwa na Fundi Maico yatarajiwa viwango vyake vya uimara( strength) ya msingi na ukuta vitakuwa si mujarabu hivyo kuezeka nyumba hii kwa G28 inaweza kupeleka uzito mkubwa unaoweza kuhatarisha maisha ya nyumba yako. Vile vile kama hali ya hewa ya udongo, maji kutwama, mmomonyoko n.k vyaweza kupelekea nyumba kutitia.
Hii ni muhimu kwa sababu Bando la bati 16 , G28 lina karibu uzito wa kilo 92 wakati bando la bati 16 G30 lina uzito wa takribani kilo 50. Kwahiyo nyumba kubwa kama shule, godauni, kanisa au hospitali utajenga kwa bando ngapi na huo msingi na ardhi vitahimili hizo tani za uzito wa paa??
3. Teknolojia ya uezekaji. Hii inaenda sambamba na ukubwa wa jengo. Nyumba zetu hizi kenchi hadi kenchi ni mita moja tu au chini ya hapo. Shule na kanisa au msikiti vipimo ni vikubwa zaidi so yafaa G28.
Kuhusu Bei za Mabati kutofautiana.
Katika uchunguzi wangu nilifikia hitimisho kuwa hakuna tofauti kubwa ktk bei na utofauti wa bei haumanishi yenye bei kubwa ni imara na bora zaidi. Fuatana nami:
Wauzaji wengi watakueleza kuhusu Gauge ya bati, rangi, na urefu na bei kamwe hawakwambii upana wa bati.
Mfano. Kiwanda cha tabata bati la G30. Migongo mipana( msauzi) urefu futi 10 linauzwa elfu 30. Bati hilo hilo Kiwanda cha Bati Bomba wanauza elfu 28,500. Lakini ni hivi upana kwa Tabata ni 750mm wakati BatiBomba ni 90mm. Vivyo hivyo Sunshare bati zao upana ni 870mm na wanauza elfu 34,500 kwa bati hilo hilo la urefu futi 10, G30 na rangi ile ile.
Kwa G28 Batibomba wanauza futi 10 migongo mipana kwa 34500 wakati ALAF wanauza takriban 55,500. Unaweza kudhani Alaf wanauza bei kubwa sana lakini ALAF bati zao upana ni 1220mm wakati Batibomba ni 900mm. Hapa utaona kuna tofauti kubwa sana. Uki converge hizi factors kwa pamoja utakuta wote bei karibu sawa.
Mfano huo huo unaenda kwa Sunshare na Tabata.
So utahitaji kununua mabati machache ALAF a utahitaji mabati mengi Sunshare.
Jambo lingine linaloweza kuchangia utofauti wa Bei( usihusishwe na ubora au uimara) ni miundo mbinu ya uzalishaji mali pamoja na rasilimali watu.
Mfano. ALAF wana majengo mazuri ya kisasa ya kibiashara full kiyoyozi na ukifika pale kama uko nyumbani au ofisi ya CAG Kichere. Wakati ukifika Tabata na Batibomba joto na vumbi mwendo mdundo wanazalisha kwenye magodown hapo hapo ndio wateja wanachukulia mizigo yao. Hawa watu hawawezi kuchaji bei sawa. Lazima bei za pango na mandhari mazuri uyalipie. Hivyo hivyo kwa Makampuni mengine.
Ushindani wa kibiashara: makampuni mengine nje ya ALAF ni mapya na mageni. Hivyo wanaunafuu kidogo kutokana na mahitaji ya kujitangaza na kujitanua. ALAF tayari ni mkongwe wajenzi wa viwanda na serikali inachukua mizigo mikubwa kwake. Hana shida na hizo milioni zako 2,3, 4, 5...
Kuhusu Malighafi
Wote wananunua kwa supplier wanaofanana. Aidha South afrika au China na india. Na wote mali zao huingizwa zikiwa tayari zimeshachanganywa materials na Rangi. Kazi yao hapa Dar ni kukata na kukunja muundo unaotaka IT4, IT5, Versatile, Romantile....etc.
NB: mimi sio Injinia wa ujenzi wala sina any formal profession kwenye industry hii. Hii ni kutokana na elimu ya hapa na pale niliyodanya mimi mwenyewe kwa kuona, kuuliza, kushika na kusikia viwandani.
Penye makosa/ mapungufu wataalam karubuni kurekebisha.
Unora kiaje sio kuja na maelezo ya jumla jumla tuu.Bati moto ni za kampuni ya kichina inaitwa Dragon! Wana mabati safi sana sana! Kampuni hii in branches zake Mbeya, Makamako, Dar, na baadhi ya mikoa! Ni mabati mazuri sana Dragon! Au nimesema uongo ndugu zangu!
Sawa mkuu Abdul nitakuja hapo baadae nadhani by August tutawasiliana.Tafadhali tutembelee na sisi uje kujionea vifaa vyetu vya kuezekea na ujenzi wake. Ni tofauti na hao wote uliowatembelea. Tunajivunia ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.
Karibu sana, namba zangu ni 0625249605.
Nilichukua mzigo Dragon mwaka jana. Nitaendelea kuwa shahidi mwaminifu kutia ushuhuda. Kuna watu walinitisha eti baada ya miezi sita zitachuja. Bado ni mpyaaaBati moto ni za kampuni ya kichina inaitwa Dragon! Wana mabati safi sana sana! Kampuni hii in branches zake Mbeya, Makamako, Dar, na baadhi ya mikoa! Ni mabati mazuri sana Dragon! Au nimesema uongo ndugu zangu!
Acha kutisha watu bati sio dhahabu kiasi hichoUkichukua bati kiwandani ALAF hakikisha unafanya escort mwenyewe mpaka site na wakati wa kupaua uwe hapo hapo ukikwepesha macho kidogo tu watu wanaingia nayo buguruni wanabadilisha faster unakua umepigwa
Sawa mkuu Abdul nitakuja hapo baadae nadhani by August tutawasiliana.
Karibu sana.Sawa mkuu Abdul nitakuja hapo baadae nadhani by August tutawasiliana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Tuulizane tu hapa hapa. Wasiojulikana bado hawajaisha wameenda likizo tu.
Muonekano wa kuezeka kwa vifaa vyetu ni huu...Nimeshazijua hizo nyumba za mabati yasiyoonekana. Zipo kama misikiti!
Na kwa ndani ni muonekano huu👇🏿
Endelea kufafanuaNa kwa ndani ni muonekano huu👇🏿View attachment 2261174
Hapo umepunguza gharama za mbao za kuezekea, umepunguza gharama za mabati, umepunguza msongamano wa mafundi, umepunguza gharama za mbao za kupigia gysum boards, umepunguza gharama za gysum boards, umeokoa nafasi kubwa ya kipaa. Na kama ulianza kujenga kwa msingi mzuri na ukajenga kuta kwa tofari zenye uimara unaokubalika, unakua umeshapata kiwanja kingine (ghorofa) juu ya nyumba yako.
Abraar Bricks Nyumba kwa Wote. Ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0625249605.