Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Kama hutajali naomba uwe mpenzi wangu tuanze safari ya kufikia lengo kuu la kuwa mume na mke, ni ombi tu
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Ila Nifah.....
 
Sema ukweli, alikuvumilia sana, kijana wa watu. Una lipi la kueleza kwa singp maza wakipata kijana ambaye hana mtoto kama jamaa
 
Humu pipo zinapenda zenyewe zikinanga kusema au kuchamba mtu mtu atulieee tu ndio zinafurahia tena kwa kumchangia kabisa yanii utulieee tu ..Huyo mtu akijibu na ameharibu uzi bwahahahahahahahahah!
Nifah Nimeipenda Hii akili big up
 
Sasa kama Jamaa alianza kwa kupenda avatar yako kabla ya kukuona uliamini mtatoboa?
Alafu we ndo tatizo mambo ambayo ulitakiwa kuyamaliza huko faragha na muachane kwa amani unakimbilia ku publish we ni mwanamke unaependa drama huwezi kutunza siri.
 
Back
Top Bottom