Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mahusiano yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mahusiano yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mahusiano ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika safari ya maisha yake mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Pumbafu weee
 
Bado hawajaanza, ila wanashangilia mno huko waliko,..wanaomba babu trump afanye kweli... matokeo yake ndo haya watu presha 😭😭
Afanye kweli nataka niwaone wazee wa kula tunda kimasihara suruali zinavyoshuka viunoni na kubaki vichwa vikubwa km siafu..!! 😹😹
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mahusiano yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mahusiano yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mahusiano ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika safari ya maisha yake mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Ni Kwanini AMEKUACHA?
 
Ni wakati wa kutulia sasa, usiingie kwenye mahusiano mapya haraka haraka, mapenzi ya kweli hayahitaji haraka, nakuombea upate mtu mwingine aliye bora ambaye mtafunga pingu za maisha na kutengeneza kizazi kijacho.
Huu ushauri si mahali pake humu. Unataka sasa asinanii harakaharaka akae nazo hizo niege mpaka lini? Acha hizi wewe
 
Back
Top Bottom