Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Acha unaa mkuu! Unatuharibia
Unaa upi? Nimempa ushauri kwasababu ana tabia njema na anahitaji mwanaume mwema wa shoka, atakayemuongoza na kumlinda.
Akiwa na haraka hatampata kabisa na anaweza kuwa single mom.
Kuna wanaume huwa wanawapeleka wanawake katika wrong direction na wapo wanaowapeleka katika right direction ( ndoa, kujenga familia).
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Naona wakwe,ndugu upande wa kike na kiume tumepewa taarifa.

I love JF.🤣
 
Mdogo wangu 🤣🤣🤣😊
 
Back
Top Bottom