Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Shemela si ungekausha tu, HivI vile umekuja na uzi inaonekana anayeumia ni wewe huku mtaalamu bold Yuko katulia zake na manzi mwingine kimya Wala Hana habari.
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
 
Kwa hiyo unataka mwenzako apange msururu hapa kila mtu aujue[emoji1787][emoji1787], bora akawa na privacy tu manakeeee..
Haha hapana huyu wa sasa alisema mwenyewe kwamba kuna siku atamuweka wazi, sasa naona leo anakuja na habari za kutokuweka tena wazi mahusiano yake, ndio nataka nijue je hili tamko linajumuisha na huyu wa sasa au watakaofuata
 
Hii taarifa najua ni ya kuhuzunisha ila haya mafataki ya mwaka mpya yanafanya nashindwa kucatch feelings[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


Ila mods imagine mtu anatoa taarifa ya kifo halafu ndo haya mafataki yamekakamaaa

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukisoma comments humu ni kama vile watu wamefurahia hao wawili kuachana.

Hii itapelekea wengine kuogopa kuweka wazi mahusiano yao humu.

Na mnafanya na sisi Wazee wenu tuogope kuwatambulisha Bibi zenu kwa kuogopa mtatuchawia tuje kuachana Uzeeni [emoji12][emoji119]
Kiukweli kabisa...jf sio sehemu ya kuweka mambo yako sio ya mahusiano tu hata mengine yahusuyo maisha binafsi
 
Back
Top Bottom