Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Yaani kisa umeumizwa na mmoja ndio unachukia mapenzi?Mapenzi ni kitu kizuri ila sio Kila penzi lazima lilete matoleo chanya,mengine ni njia tu,mengine ni lesson ila Kuna muda utampata mtakayefanana,,,HUNA sababu ya kuchukia mapenzi.....ona mfano wa Nifah Yuko very strong,and that is how it should be
Sawa nipo na vitu mingi ya kufanya wacha Munge aseme
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
. Pole sana mkuu, 😟


. Ila Mkuu tuaze lini kutuma maombi mapya 😐
 
Back
Top Bottom