Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah
Moyo ni wakò una uhuru uchague mahali salama.
Ninaamini umefanya maamuzi sahihi, nijuavyo mtu kamwe hawezi kuacha kitu cha thamani, hivyo kama mapenzi yameisha, uko huru kumchagua umpendaye.
Asikusumbue mtu kwa kejeli...kuwa imara, humu watu wananuka matatizo wanataka pa kumua
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Mara nyingi wapenzi hushindwa kuukubali ukweli kwamba safari yao imefika mwisho. Hivyo pamoja na kuwapa pole kwa kutengana inabidi pia niwapongeze kwa kuchukua maamuzi hayo magumu. Nawaombea furaha ya kweli na muishi maisha ya kutojutia uamuzi wenu.
 
Mnatuchanganya huyu ndio huyo BOLD au Kuna njemba nyingi maana maneno haya yana ukakasi

BOLD mmeachana August 2023

Huyu mlieachana mkarudiana mpk sasa hivi mambo ni burudanii ni nanii?

Najaribu #$najaribu, microphone test View attachment 2858971
Unajichanganya mwenyewe, niliyeachana nae August namuongeleaje Nov?

Huyo ni mpenzi wangu wa sasa, usipoelewa subiri kuna siku nitamuongelea kwa kina.
 
Nifah
Moyo ni wakò una uhuru uchague mahali salama.
Ninaamini umefanya maamuzi sahihi, nijuavyo mtu kamwe hawezi kuacha kitu cha thamani, hivyo kama mapenzi yameisha, uko huru kumchagua umpendaye.
Asikusumbue mtu kwa kejeli...kuwa imara, humu watu wananuka matatizo wanataka pa kumua
Maneno yenye hekima tele, asante sana.

Mungu ananiongoza, amenipa kilicho bora Alhamdulillah 🙏🏽
 
Uzuri umefundwa sana. Unazingatia ushauri wa mafiga matatu au ndoo kubwa na kidumu cha mkononi. Yaani wakati The Bold anazingua mwingine alikuwa alikuwa anatest mitambo.😂😂😂🏃‍♂️🏃‍♂️
Kongole
Hapana jamani, nilipambana mwenyewe na wala kaka mzuri hakuwa na taarifa ya chochote hadi tulipoachana kabisa na mimi kukaa sawa ndipo akaingia yeye 😊
 
Hapana jamani, nilipambana mwenyewe na wala kaka mzuri hakuwa na taarifa ya chochote hadi tulipoachana kabisa na mimi kukaa sawa ndipo akaingia yeye 😊
Aisee hata ungetangaza jimbo liko wazi nisingeweza ushindani sina vigezo. Ila wanaume tunachapiwa sana The Bold naye atangaze ule mchepuko uliowasambaratisha😂😂
 
Back
Top Bottom