Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858946
If you love something, let it go
If it comes back to you, it yours
If it doesn't , you never know.
Acha hizi mambo. Ng'ang'ana, shikamana, komaa. Wakati mwingine Malaika mleta riziki haji mara nyingi. Akipita amepita.

Nakukumbusha ..tuu. haya waachia Akina Maya Angelou. Ya kwenye vitabu haya. Sounds profound ila si uhalisia.

Heri ya 2024.
Ukashikamane haswa
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Shusha ubuyu wake sasa kama unavyoshushaga wa wengine. Vipi jamaa hasimamishi nini na hawezi fanya kazi au jamaa ni punga kama unavyozushiaga wengine?😀😃😄😁😆😅
 
ilawewe😁juzituu hapa kunamemba anaitwa mdukuzi aliweka uzi wakumtema mpenzi wake amekuja kupanga chumba kimoja maskini akitokea Tabata watu tukahisi niwewe ndio umetemwa



akaja mdakuzi kumuelewesha DEPO mana alikuwa anahisi wewe ndio umeachwa.

mdakuzi alimuambia DEPO "pole kwakushindwa kututofautisha" ulipo iona ile comment ukamuambia mdakuzi "polehio vipi beby?"
nijuzi tuu hapo hata wiki haijaisha leohii unasema mliachana kitambo?mbona muongo hivyo?
Japokuwa umejikanyaga ila nimekusoma kwa umakini umenipa kitu ambacho nilikuwa sikijui!

Niliyeachana nae ni wa zamani na nimetoa taarifa rasmi maana niko na mwingine, huyu mpya bado ninae na tunapendana ileile.
Tulia sasa
 
Back
Top Bottom