Nifanyaje ili niache kupanga? Kipato 400,000 kwa mwezi

Nifanyaje ili niache kupanga? Kipato 400,000 kwa mwezi

hhhh.jpg

Igawe mara tatu

1/3 = Matumizi binafsi (nauli/msosi/vocha, chenchi ndogo ndogo eka kwa kibubuu etc)

1/3 = Akiba (lengo kubwa likiwa ujenzi) --- nkikustukizia na mimi sijajenga... sitakupa lift hata ka wanyeshewa mvua ama jua kali

1/3 = matumizi ya kijamii (zaka, michango muhimu kwa ndugu, ya kuhonga vitu vidogo vidogo, chenchi ndogo ndogo eka kwa kibubuu etc)
(1/3+1/3+1/3 = 1 = 400,ooo)

*Uwe mwaminifu katika hesabu ulizojiwekea
 
Kama una wategemezi, tufanye unaishi nao nyumbani.
Piga budget ya elfu 5 kwa siku. Wapike chakula nyumbani.
Kwa mwezi ni laki na nusu.

Wewe chai utakunywa nyumbani na dinner, lunch utakula kazini isizidi 2000 kwa siku. Kwa mwezi 50000.

Jumla 200k. Baki 200k.

Sasa hapa inabidi usave 100k kwa ajili ya ujenzi na 100k kwa ajili ya dharura kila mwezi.

Hapa utaweza kujenga kama una kiwanja tayari na utaanza kidogo kidogo.

Pia tafuta kazi za ziada za ku raise kipato chako. Kama umeoa na mke ajishughulishe ili aweze kukusaidia majukumu ya nyumbani mfano chakula nk.
 
Sikushauri ujenge kwa kipato hicho,cha kufanya tafuta kipato cha ziada ambacho kitakuwezesha kupata mahitaji yako ya kila siku.Huo mshahara ukopee,pandisha nyumba yako,paua then malizia vyumba viwili hamia,sehemu iliyobaki utamalizia ukiwa hapo.Hii pia itasave hela ya kodi.Kutafuta kipato cha ziada sio lazima uwe na biashara kubwa,hata ukiuza ice cream kwenye shule yenye watoto wengi kwa siku unaweza pata faida sh10,000 na zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemeana na mahala ulipo. Kwa mkoani,hiyo unajenga hata chumba+sebule+chumba mnahamia. Lakini kama uko mnakobanana dar,hiyo itabidi ujinyime sana mkuu,ukanunue kiwanja huko nje ya mji cha milioni hata 5

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka mshahara wake wa mwaka mzima ni 4.8mil, so hapo unaweza kuelewa ili apate hio 5mil inaweza kumgharimu muda gani boss.

dodge
 
Back
Top Bottom