Nifanyaje kuzuia matangazo kuingia kwenye simu yangu wakati wa kutafuta kitu kwenye Browser

Nifanyaje kuzuia matangazo kuingia kwenye simu yangu wakati wa kutafuta kitu kwenye Browser

Kuboma

Senior Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
154
Reaction score
189
Wakuu

Nifanyaje kuzuia matangazo kuingia kwenye simu yangu wakati natafuta kitu kwenye web browser

Nawakilisha hapa nashindwa hata kuandika
 
Nimewahi kupatwa na hilo tatizo. Lilikuwa sumbufu sana.
Nilipitia app zote na kufanya setting upya bado tatizo liliendelea.
Chrome mda mwingine wanazingua sana. Dawa pekee ni kwenda kwenye storage kufagia mauchafu yote
 
Nenda kwenye account yako ya google(email) ufanye hayo marekebisho.

Hawakati bila wewe kuruhusu, ulisharuhisu na ukaweka detail zako kua wakate wapi ili kulipia huduma.

Au labda una zile app za kulipia kama wps au youtube na umeset wakate pesa kila baada ya siku, wiki au mwezi.

Nenda playstore, ingia kwenye account yako halafu ingia pale payments and subscription ukaedit ulivyoviweka.
 
Kama unatumia edge,firefox,yandex,opera mini unaweza kuadd extension ya kuzuia matangazo ila kwa chrome hii feature ipo kwenye desktop tu bado kweny android hawajaiweka labda matoleo yajayo
Screenshot_20250302-092823_Edge.jpg
 
Nenda setting kwenye simu yako, ingia kwenye upande wa connections tafuta neno limeandikwa private DNS, kama hujaliona ingia kwenye maandishi ya more connection settings na utaona maandishi yaliyoandikwa private DNS.

Baada ya kubonyeza hilo neno la Private DNS, yatakuja maneno matatu, Off, Automatic na Private DNS Provider Hostname.

Bonyeza katika Private DNS Provider Hostname na kwachini yake utaandika maneno yafuatayo,

dns.adguard.com

Kisha bonyeza save.
Faida:
Ita blocks ads kwenye browser zote na pamoja na ads za kwenye Apps zote za simu yako, hivyo hautapata tena usumbufu wa aina yoyote ya matangazo sehemu yoyote ya simu yako.
 
afuate ushauri huu
 
Wakuu

Nifanyaje kuzuia matangazo kuingia kwenye simu yangu wakati natafuta kitu kwenye web browser

Nawakilisha hapa nashindwa hata kuandika
Mkuu watu wapo web3 siku hizi.

Achana na hizo broweser nyingine kama Chrome au Firefox, ingia playstore kisha download browser inaitwa BRAVE, hutojutia hautaona tangazo kwenye site yoyote unayotumia.
 
Mkuu watu wapo web3 siku hizi.

Achana na hizo broweser nyingine kama Chrome au Firefox, ingia playstore kisha download browser inaitwa BRAVE, hutojutia hautaona tangazo kwenye site yoyote unayotumia.
Mwamba nimekukubali ungekuwa kalibu ningekupa zawadi,yaani simu imenisumbua kwa siku 2 kila sekunde zinaingia Aplication
 
Njia pekee ya kuepuka usumbufu wa adds ni ku restore Kila kitu uanze setting upya..
 
Back
Top Bottom