Nenda setting kwenye simu yako, ingia kwenye upande wa connections tafuta neno limeandikwa private DNS, kama hujaliona ingia kwenye maandishi ya more connection settings na utaona maandishi yaliyoandikwa private DNS.
Baada ya kubonyeza hilo neno la Private DNS, yatakuja maneno matatu, Off, Automatic na Private DNS Provider Hostname.
Bonyeza katika Private DNS Provider Hostname na kwachini yake utaandika maneno yafuatayo,
dns.adguard.com
Kisha bonyeza save.
Faida:
Ita blocks ads kwenye browser zote na pamoja na ads za kwenye Apps zote za simu yako, hivyo hautapata tena usumbufu wa aina yoyote ya matangazo sehemu yoyote ya simu yako.