Pole sana mkuu.
Katika makosa yote ambayo hupaswi kumsamehe mwanamke ni CHEATING. Mwanamke msaliti hasameheki, sababu ya kutosameheka ni moja tu, hatoweza kuacha kurudia hiko kitendo cha kusaliti, either umejua au hujajua ila ataendelea tu na huo mchezo.
Tunza hizo picha sehemu kadhaa, kaa nae chini na umwambie mmefika mwisho wa mapenzi yenu. Achana na machozi atakayotoa, achana na maneno ya kujishusha na kuomba msamaha atakayotoa, ni hisia tu hizo ila ukishamrudisha ktk nafasi yake baada ya muda atasahau.
Tunakwambia hivi sababu tayari tumewahi kupitia mazingira kama yako, mwanamke aliyetolewa mahari au anakaribia kutolewa mahari hapaswi tu kucheat ila hata kuwaza kucheat hapaswi kabisa kuwaza. Dalili zote unazoona kwenye uchumba, ndani ya ndoa inakuwa ni mara mbili yake.
Tafuta humu wanaume waliowahi kusamehe wapenzi wao kwa kesi za cheating je, wake zao walibadilika?