Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Mil 1 umepima iyo kiasi ukaona lazima italeta profit ya laki 2 per week, sema inawezekana kama utauza highly consumable goods, naamini still 1mil. ni kubwa, mtu akisema anahitaji 10mil au 5mil afanye biashara iyo ni kufikiri kutaka kuwa comfortable zaidi.. lakini out of comfortable zone unaweza kufanya business kwa kiasi chochote hata cha chini na uwe comfortable... 1mil. Ukiweka usharobaro mbali ni kubwa tu. Be inspired, push it, awake, be confident, never get tired, become only positive, if you stay positive in negative situation then you win, tambua most of the people they will be negative ukiwa unaanza hapo uwe makini, ukifanikiwa watakuhitaji, waambie mwanzo if you don't love me now don't love me later when my paper is much......
 
Nunua handbags za kike, classic ,inakaa pc tatu au nne, znakuwa tofaut kabsa na zile zinazouzwa kkoo... Unanunua kwa 17,000 usafir 3500 kila handabag, jumla 20500...
Ww uza 28,000 jumla

Maana huku jumla wanauzaga 35 rejareja 40 hadi elfu 60..

Ukipost mitandaon utapata wateja kutoka mikoa weng na hapa dar kwa ajili iyo bei ndogo.

Kuuza handbags 20 kwa siku n kitu cha kawaida kabsa..

Au unawauzia wenye maduka unachukua order
Unapofata mzigo wa handbags unachanganya na vichwa vya kuuzia mawigi vinauzwa 1700 usafiri wa kila kochwa 2000 jumla 3700 kikifika Tanzania huwa vinauzwa 15,000 hadi 20,000

Pia changanya na midoli ya kuuzia nguo,
Inauzwa 17,000 usafiri 17,000 jumka 34,000 hapa tanzania inauzwa elfu 80 hadi 150,000.

Ningekuwa na capital mimi ningekuwa tajiri tayar daaa maana machimbo ya hivi vitu nayajua vzur

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo wapi mkuu? Unaongelea kutoa uganda, au?
 
Kijana acha tamaa.

Anza kidogo kidogo,
kuwaza vikubwa wakati hata vidogo huviwezi ni hatari na UTAPOTEA.

Kwa kijana mpya asokua na uzoefu wa biashara.

Kwa huo mtaji wa million Moja,
Faida yake inastahili kua elfu 20-30 kwa wiki.

NB: Hiyo faida (Mapato-Matumizi) ya laki 2 kwa mtaji wa million Moja ni Ndoto.

Vinginevyo unaongelea MAPATO ya laki 2 kwa wiki.

Kiuhalisia,
Kama unataka Faida ya Laki 2 kwa wiki,
Itakubidi uwe na MAUZO yasopungua Millioni 2 kwa wiki.

Sasa,
MAUZO ya million 2 wakati Mtaji wako ni Millioni 1 ni KICHEKESHO CHA MWAKA itakua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafuatilia huu mjadala bega kwa bega " ijapokuwa ulinipita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom