Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Kama una eneo kubwa, fuga hata kuku wa kienyeji, ukiwa na usimamizi mzuri laki 2 unapiga ndani ya wiki kirahisi
mkuu mimi nafuga kuku wa kinyeji sio rahisi kama unavyosema. inahtaji uwekeze kwenye na ujifunze kila eneo kuanzia kujenga mabanda , kuzuia magonjwa, lishe sahihi, na usubiri miezi sita wakue ndipo uwauze au kama unaze kupata mayai ikiwa umefuata taratibu sahihi zinazotakiwa na kwa kwango cha chini wawe angalau 150 .. ungesema wa kisasa wa nyama hao mzunguko wao ni mfupi ndani ya wiki nne umewauza lakini wanataka uangalizi wa hali ya juu sana na umakini na soko la uhakika na ufuge kuanzaia 1000
 
Naendelea kupitia huu uzi kuna hali nimeiona wacha nifunguke. sio kwamba watu WANAPIGWA ni kuwa wao wenyewe WANAJIPIGA maana hakuna kinachoendelea isipokuwa tumekiruhusu wenyewe kitokee.
kuna mtu anaitwa PAVLOV (1902) alifanya utafiti akawa kila akimpeleka mbwa chakula anapiga kengele. siku hiyo akapiga kengele bila kupeleka chakula mbwa akaanza kuhangaika na kushusha mate maana alikuwa anajua kengele ikilia tuu msosi unakuja kwa hiyo kuna hali ya kubebwa na hisia bila kufikiria kwa kina ili kuweza kufanya maamuzi. sio kwamba ukiona mtu anapata katika eneo fulani na wewe unaweza tuu kuingia kufanya USIWE MBWA WA PAVLOV unahitaji kufikiri kwa kina na kufikiria kila kitu kabla hujafanya maamuzi. kwamba watu wanafanikiwa kufuga sungura au samaki au kulima tikiti au mapapai au kuwa ma mc au kuuza chipsi na wewe uende ukafanye.
 
Muda, commitment, determination, goal setting(unataka kufikia nini, lini na vipi), resources, location, market research na partner ambaye mna same vision and commitment, above all, Love what you do, usifanye kwa ajili ya watu au kwa ajili ya shida.
Doh! Hivyo vigezo vyote nipo vizuri lakini ninashida pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mimi nafuga kuku wa kinyeji sio rahisi kama unavyosema. inahtaji uwekeze kwenye na ujifunze kila eneo kuanzia kujenga mabanda , kuzuia magonjwa, lishe sahihi, na usubiri miezi sita wakue ndipo uwauze au kama unaze kupata mayai ikiwa umefuata taratibu sahihi zinazotakiwa na kwa kwango cha chini wawe angalau 150 .. ungesema wa kisasa wa nyama hao mzunguko wao ni mfupi ndani ya wiki nne umewauza lakini wanataka uangalizi wa hali ya juu sana na umakini na soko la uhakika na ufuge kuanzaia 1000
Vipi kwa mtu anaenda kuwanunua mkoani mfano Tabora,Singida,Bahi,Manyoni, Tanga na kwingineko akaja kuwauza mjini, mbona nahisi kama vile kuna faida kubwa kuliko kuwa mfugaji?.Mkuu naomba maelezo kidogo juu ya hili nazungumzia kuku wakienyeji.
 
mkuu sijawahi kufanya biashara hiyo ila tatizo kubwa ninaloliona kwa hao kuku ni kuwa huwa wanauzwa kwa wingi ule msimu wa magonjwa ya mdondo pamoja na ndui. hivyo kama utawanunua na kuwapa chanjo stahiki na dawa za minyoo na kukaguliwa na daktari wa mifugo ukasafirisha utafanya biashara nzuri.
 
Back
Top Bottom