Nifanye nini? Nataka mume wangu aumie kama ninavyoumia mimi

Nifanye nini? Nataka mume wangu aumie kama ninavyoumia mimi

kwahiyo wewe ukajua ndoa ni free style😂😂😂. Ndio maana zikaitwa ndoa za mchongo sikuizi, wewe nani kakwambia ukiolewa unaishi kama msela. Sasa siubaki bachelor tujue. Simwanaume wala mwanamke wote wapo kifungoni. Ndoa sio dating wala courtship 😂😂

huyo mwanaume ndio anaishi kama msela na si kweli yuko kifungoni, anafanya analotaka, huyu mwanamke ndio yupo kifungoni.

Eti ndoa sio dating wala courtship, hujielewi mkuu...au wewe ndoa yako ilikua ya mkeka,uliozeshwa tu? na hujui hizo ni process tu za kuelekea ndoani.
 
Halafu kuchepuka kwa mwanamke kunamwisho labda awe anajiweza hivyo aanze kulea watakaochepuka naye. Huyo mwanaume mjinga wakuoa mdada wa kujirahisisha siatakuwa mjinga. Wewe mwenyewe mdada utajishtukia. Pia, uzinzi ukifika kipindi utakuchosha tu. Kila siku unachukuliwa kama tambala bovu kwakujirahisisha, utajiona mpumbavu umri wa utu uzima ukiingia balaa. Ujana maji ya moto.

nishaona watu kibao wameachika na kuolewa, ndoa sio kifungo uvumilie kila aina ya ushenzi, kisa kujirahisisha ndio watu wanatafsiri ndio kuchepuka, mtoa mada chepuka unaweza kupata anayekufaa....usiogope kamwe ku 'experiment' huko nje,kunaweza kukafaa zaidi.SIO wanaume wote wanachepuka hadi na ndugu wa mke, wapo good men,is you to find them.
 
Uyo mfanyie kitu kama cha Felix wa Jua kali alichomfanyia baba yake Mr. Thomas

😎Reference JUA KALI(dstv )Maisha magic Bongo
 
Kama unachepuka na bado unawaza kumuumiza mmeo, basi ujue mchepuko hajafika levels za mumeo. Ukipata mchepuko unaemuelewa, habari za mume huzikumbuki kabisa.
 
Wewe chepuka kwa starehe zako kama yeye anavyofanya....vinginevyo unatafuta kudedi
 
huyo mwanaume ndio anaishi kama msela na si kweli yuko kifungoni, anafanya analotaka, huyu mwanamke ndio yupo kifungoni.

Eti ndoa sio dating wala courtship, hujielewi mkuu...au wewe ndoa yako ilikua ya mkeka,uliozeshwa tu? na hujui hizo ni process tu za kuelekea ndoani.
Sasa nawewe siunaona tayari kashairibu ndoa yake au wewe unavyoona nisawa. Mwenzako akiharibu sepa, chakujiumiza nini. Ndoa nikifungo, mtu yeyote akikivunja ndoa imevunjika. Mimi naongelea ndoa iliyotulia wewe unanitolea mfano wa ndoa iloyokufa, tupo sawa kweli😂😂😂
 
nishaona watu kibao wameachika na kuolewa, ndoa sio kifungo uvumilie kila aina ya ushenzi, kisa kujirahisisha ndio watu wanatafsiri ndio kuchepuka, mtoa mada chepuka unaweza kupata anayekufaa....usiogope kamwe ku 'experiment' huko nje,kunaweza kukafaa zaidi.SIO wanaume wote wanachepuka hadi na ndugu wa mke, wapo good men,is you to find them.
Sasa unaexperiment ndani ya ndoa halafu still uiite ndoa, we mzima kweli. Umeshaingia ndani ya ndoa, eti unafanya process ya kuingia tena ndani ya ndoa kabla ya kujitoa kwenye hii😂😂😂.

Sasa hiyo sio experiment bali inaitwa uasherati. Watu hawaexperiment ndani ya ndoa bali mnaishi, ndoa ikivinjika toka kaexperiment. Sasa mwenzako anang'ang'ania kote. Kwakweli TZ tuna mental disorder 😂😂😂.

Sianataka kuexperiment, basi atoke ndani ya ndoa. Sasa mwenzako kacheat nawewe unacheat badala ya kusepa, mbona akijiua wewe hutajiua😂😂😂. Aisee wadada maisha sio kucopy na kupaste pia mabaya mawili hayafanyi moja liwe zuri. Tunasafari ndefu😂😂. Mwishowe muuwane.
 
Sasa nawewe siunaona tayari kashairibu ndoa yake au wewe unavyoona nisawa. Mwenzako akiharibu sepa, chakujiumiza nini. Ndoa nikifungo, mtu yeyote akikivunja ndoa imevunjika. Mimi naongelea ndoa iliyotulia wewe unanitolea mfano wa ndoa iloyokufa, tupo sawa kweli😂😂😂

sasa tunachobishana ni nini,kumbe unajua mwenzio akiharibu sepa, sasa kwa nini mnamshauri huyu dada akae,naona nazunguka mizungu, baki na msimamo wako usiojulikana ni upi.
 
Sasa unaexperiment ndani ya ndoa halafu still uiite ndoa, we mzima kweli. Umeshaingia ndani ya ndoa, eti unafanya process ya kuingia tena ndani ya ndoa kabla ya kujitoa kwenye hii😂😂😂. Sasa hiyo sio experiment bali inaitwa uasherati. Watu hawaexperiment ndani ya ndoa bali mnaishi, ndoa ikivinjika toka kaexperiment. Sasa mwenzako anang'ang'ania kote. Kwakweli TZ tuna mental disorder 😂😂😂. Sianataka kuexperiment, basi atoke ndani ya ndoa. Sasa mwenzako kacheat nawewe unacheat badala ya kusepa, mbona akijiua wewe hutajiua😂😂😂. Aisee wadada maisha sio kucopy na kupaste pia mabaya mawili hayafanyi moja liwe zuri. Tunasafari ndefu😂😂. Mwishowe muuwane.
wewe una mpango tu wa kubishana, experiment ni uasherati, ila huo anaoufanya mumewe sio uasherati?? au kunya anye kuku akinya bata kaharisha, hapa usizunguke mibuyu tunachoshauri ni huyu dada amove on, kama umenisoma posti yangu ya kwanza nimeshauri aachane na mumewe, sijui unaniquote ili iweje??? chukua time huko
 
Mwanamke hatulii hadi ajitulize.

You are so powerful enough to heal yourself. YOU ARE A WOMAN you are strong enough to handle it.

Punguza matarajio na ikibidi yaondoe kabisa kwa mumeo.
Inner management your healer.

Jisikilize wewe utapata mambo mawili utulivu wa akili (uhakika na udhibiti).

Keep yourself busy,.
Tafuta AMANI itakuletea FURAHA.
 
Dah... poleni sana wake zetu, labda nikushauri uache tu kumchunguza mumeo, ipo siku atabadilika, mimi hapa nilikua mchepukaji balaa na ilisababisha mtafaruku baina yangu na mke wangu, nilitumia kila mbinu kumficha sema yeye naye alitumia kila mbinu kunichunguza.

Leo hii napambana sana kuepuka kuchepuka maana moyo hunisuta sana kila nikifanya hilo tendo, japo hawa wanawake wa leo yaani vigumu sana kuwaepuka, wanatumia mbinu nyingi sana kututega, kwa kweli wanaume tunapitia majaribu ya kila aina.

Nina uhakika mumeo hapo alipo anapambana sana na moyo na nafsi yake, kama ambavyo ninaumia, leo niko nchi nyingine nimesafiri kikazi, vishawishi vya kuchepuka viko kote kote ila najikaza sana kwa kila hali, sio rahisi aisei, ni tatizo kubwa sana, Mungu atusaidie.
 
Bora muachane tu msijeuana bure mkaacha watoto wanateseka. Wanaume huwa tunaumia zaidi tukisalitiwa, akijua atakuacha tu
 
Nimeolewa ndoa yangu ina miaka kumi, miaka yote hiyo nimekuwa nikiishi kwa mateso, mume wangu anahudumia familia na kila kitu, lakini ni malaya sana, anatembea mpaka na ndugu zangu.

Nimevumilia mpaka nikachoka, mwaka jana kwa hasira nikaamua kuchepuka, mwanzo nilikuwa na amani lakini sasa hivi sina amani kwani naona kama mume wangu haumii. Yeye anachepuka mimi najua nateseka lakini yeye hajui kama mimi nateseka.

Tumeshaitishwa vikao mpaka wametuchoka, nataka kumuumiza mume wangu, nataka ajue uchungu ninaoupitia, nataka kumuonyesha kuwa nina mwanaume mwingine, nashindwa nifanyeje, niache meseji au nipige picha nikiwa na mwanaume mwingine ili aone.

Nataka aumie kama ninavyoumia.
Mwambie, watoto sio wakwake!!
Aaaah ni utani tu Shem, miaka kumi!mume anachepuka,unavumilia tu, huogopi ngoma?

Ushauri wangu, wewe kuchepuka haisaidii, sie wanaume hata kama ni Malaya, mbwa tukifumania tu, atakutia panga, wewe una option mbili, Hama nyumba kama uwezo wa kifedha unao,au mnatengana,Richa ya kuishi nyumba moja,lakini hakuna kupeana kabisa,story pekee ni kuhusu watoto na vitu vyenye manufaa kwenu wawili,wewe ukichepuka,akigundua atakupiga,au kama anajua na hakufanyi kitu,hapo jua ameishakutoa moyoni,endelea na maisha yako,ukiwa peke yako na watoto.
 
Nimeolewa ndoa yangu ina miaka kumi, miaka yote hiyo nimekuwa nikiishi kwa mateso, mume wangu anahudumia familia na kila kitu, lakini ni malaya sana, anatembea mpaka na ndugu zangu.

Nimevumilia mpaka nikachoka, mwaka jana kwa hasira nikaamua kuchepuka, mwanzo nilikuwa na amani lakini sasa hivi sina amani kwani naona kama mume wangu haumii. Yeye anachepuka mimi najua nateseka lakini yeye hajui kama mimi nateseka.

Tumeshaitishwa vikao mpaka wametuchoka, nataka kumuumiza mume wangu, nataka ajue uchungu ninaoupitia, nataka kumuonyesha kuwa nina mwanaume mwingine, nashindwa nifanyeje, niache meseji au nipige picha nikiwa na mwanaume mwingine ili aone.

Nataka aumie kama ninavyoumia.
Itoshe kusema ndoa zinawenyewe.
 
Dada ukitaka mumeo aumie basi mwonyeshe mapenzi mazito sana, mnyenyekee, mdekeze na mfsnye wa kwanza kwa kila kitu.

Nikwambie tu si kwamba hajui kama una mwanaume, anajua kabisa ila ameshakufuta moyoni mwake. Ukitaka awe na wivu na wewe basi kaa katika nafssi yako kama mke
 
Tembea na jirani yako au ndugu yaake apo lazima aumie au tafuta rafiki yake jililengeshe
 
Back
Top Bottom