Nimeolewa ndoa yangu ina miaka kumi, miaka yote hiyo nimekua nikiishi kwa mateso, mume wangu anahudumia familia na kila kitu, lakini ni malaya sana, anatembea mpaka na ndugu zangu.
Nimevumilia mpaka nikachoka, mwaka jana kwa hasira nikaamua kuchepuka, mwanzo nilikua na amani lakini sasa hivi sina amani kwani naona kama mume wangu haumii. Yeye anachepuka mimi najua nateseka lakini yeye hajui kama mimi nateseka.
Tumeshaitishwa vikao mpaka wametuchoka, nataka kumuumiza mume wangu, nataka ajue uchungu ninaoupitia, nataka kumuonyesha kuwa nina mwanaume mwingine, nashindwa nifanyeje, niache meseji au nipige picha nikiwa na mwanaume mwingine ili aone.
Nataka aumie kama ninavyoumia.