Nifanye nini? Nataka mume wangu aumie kama ninavyoumia mimi

Nifanye nini? Nataka mume wangu aumie kama ninavyoumia mimi

But tukikosa amani ndani ya nyumba, ikitokea digidigi huko nje n mwendo wa "sukuma ndani" ukuni
Kabisa..
Kuna wakati mke anamnyima mumewe unyumba hadi anasababisha mumewe kuanza kuchepuka. Na mume akishaanza hayo mambo akakolea ndo anageuka kiwembe mazima!
 
Hilo ni kosa kubwa kumuonesha kuwa uko na mahusiano na mwanaume mwingine.bomu utakalolitengeneza litakuja kukulipukia mwenyewe na utateseka katika maisha yako Mpaka unakufa.ili Mumeo abadilike…unatakiwa kwanza wewe ubadilike mama😄😄inachekesha ehee..

Hakuna kitu inawatesa wanaume kama ukiwadharau..Simaanishi umkosee adabu mbele za watu au kumtukana…nope!

Hebu jipende kwanza(kama unakipato chako)mama vaa pendeza sana,nukia,wikendi jipeleke sehemu nzuri nzuri kajichanganye hukooo..make sure haumpi taarifa yoyote ya wapi unakwenda.

Rudi nyumbani kwa wakati,mpikie chakula kizuri(ale au asile wewe haikuhusu)timiza wajibu wako kama mke madam…najua inatesa mno lakini make sure humuonyeshi kuwa unamaumivu..hata akuumize vipi hakikisha haoni chozi lako..ukitaka kulia funga safari kalilie msumbiji huko halafu rudi.just mind yo f**** business atiii..

Matendo yako ndio yatakayomtesa.ukimind yo own things mama huyo masta atakuja kuteseka kuliko ulivyokuwa unateseka wewe.

Usisahau kumuombea mume wako,nenda faraghani huko zungumza na Mungu wako(katika ulimwengu wa roho wanaume wanapitia majaribu mengi sana.huwa tunawahukumu katika ulimwengu wa mwili.kitu ambacho kibinadamu hutokea)

****************
Kama unamtegemea Kwa kipato yeye ndie akulishe akuvishe..mhhhh hapa ni changamoto kidogo ukianza mabadiliko anakukomesha Kwa kutokukupatia pesa.maisha yanakuwa jehanamu ndogo.


**************
Kama unakipato chako mwenyewe,hebu acha uphaller jipende wewe kwanza mamaa
 
Andaa na mabegi kabisa ya kuondoka akishajua sababu ndo tiketi ya kuachwa
 
Akichepuka unaumia
Ukichepuka unaumia

Hakuna kitu kibaya kama kufanya jambo kwa lengo la kumkomesha mtu halafu ukaja gundua unayemkomesha hajali kitu...inakuwa ni kama unatwanga maji kwenye kinu,unapoteza nguvu na muda wako bure

Cha kufanya ni kuwa mvumilivu na kuongea na mume kuhusu kuumizwa na anayofanya,haijalishi ni mara ngapi unamwambia na anarudia...mkumbushe

Kama utaona unashindwa kuvumilia unaweza kuamua kuvunja ndoa

Po

Huu ni mlolongo,, ukiona kuchepuka kwako unaumia na kuhisi hatia Basi ujue unampenda mumeo,, acha kuchepuka maana kuchepuka kunamaanisha kupata ulichokosa ndani sasa km unaumia haina maana sasa,, mpuuze huenda akajishtukia ila ikishindikana kabisa heri ukaachana nae maana maisha aina hiyo hayafai,, mtauana
Kapeace , watu wengi sana tunachanganya kati ya upendo/wivu na roho mbaya.

Roho mbaya ni kama vile mchawi, anaweza kufanya jambo hata ambalo halina faida kwake lengo tu amuumize mwingine.

Hata kwenye mahusiano, wanaouana kisa eti wivu hawana upendo hata kidogo, hiyo ni roho mbaya tu, mwanaume anawaza alivyogaramia, halafu leo uondoke hivihivi au afaidi mwingine, anaona bora mfe mkose wote, hakuna upendo hapo.

Huyu dada hana upendo bali roho mbaya tu, ndio maana anachepuka ili mwanaume aumie, mwisho ataamua hata kumuwekea sumu ili tu lengo la kumuumiza likamilike..

Mwanaume hana roho mbaya kwa kuwa anafanya kujifurahisha yeye, sio kuumiza mtu..

Kama huu uzi ni wa kweli, na kama wanawake wengi wana akili hizi, basi mwanamke ni kiumbe chenye roho mbaya sana.
 
Pole sana mamy,achana kushindana na mwanaume ukiona huwezi kuvumilia tabia zake ni bora muachane
pia hivyo vikao unavyoitisha kila siku itafika mda watakuchoka na wote watakugeuka ndipo utakapoona uchungu wa dunia

Kamwe usishindane na mwanaume,sawa yeye anachepuka lakini siku akijua basi ndo mwisho wa ndoa yenu je umeshajiandaa kuachika?

Kuwa na msimamo ni muhimu kuliko hicho unachowaza kufanya,unaharibu hata amani uliyonayo inamaana umekosa vitu vya kukupa furaha tofauti na huyo malaya?

Kama mwanamke anayejitambua ulitakiwa umpuuze ila kadiri unavyozidisha kelele na kumshitaki ndo unamchochea,anayehitaji kubadilika ni wewe shida unayo wewe

Alafu dada inaonekana we ndo unamkimbiza mmeo kwa makelele yako,haiingii akilini mtu anahudumia familia alafu mfikie huko bado anaakili zake sema kuna shida mahali
 
Anakusubiria tuuu siku ajue ndo mwisho wenu maana kama anaweza tembea mpk na nduguzo kukuacha sidhani kama ni shida kwake..so natafuta sababu ya yy kukuacha,ingekua mm ww na nina ushahidi ningemuacha mimi haraka maan kuacha hakuumi kama kuachwa
 
Kapeace , watu wengi sana tunachanganya kati ya upendo/wivu na roho mbaya.

Roho mbaya ni kama vile mchawi, anaweza kufanya jambo hata ambalo halina faida kwake lengo tu amuumize mwingine.

Hata kwenye mahusiano, wanaouana kisa eti wivu hawana upendo hata kidogo, hiyo ni roho mbaya tu, mwanaume anawaza alivyogaramia, halafu leo uondoke hivihivi au afaidi mwingine, anaona bora mfe mkose wote, hakuna upendo hapo.

Huyu dada hana upendo bali roho mbaya tu, ndio maana anachepuka ili mwanaume aumie, mwisho ataamua hata kumuwekea sumu ili tu lengo la kumuumiza likamilike..

Mwanaume hana roho mbaya kwa kuwa anafanya kujifurahisha yeye, sio kuumiza mtu..

Kama huu uzi ni wa kweli, na kama wanawake wengi wana akili hizi, basi mwanamke ni kiumbe chenye roho mbaya sana.
Kwakweli tukiamua kuwa na roho mbaya tunakuwaga zaidi ya shetani
 
Hilo ni kosa kubwa kumuonesha kuwa uko na mahusiano na mwanaume mwingine.bomu utakalolitengeneza litakuja kukulipukia mwenyewe na utateseka katika maisha yako Mpaka unakufa.ili Mumeo abadilike…unatakiwa kwanza wewe ubadilike mama[emoji1][emoji1]inachekesha ehee..

Dada umemaliza kila kitu,akifata ushauri huu atakuja kukushukuru badae,
 
Nimeolewa ndoa yangu ina miaka kumi, miaka yote hiyo nimekua nikiishi kwa mateso, mume wangu anahudumia familia na kila kitu, lakini ni malaya sana, anatembea mpaka na ndugu zangu.

Nimevumilia mpaka nikachoka, mwaka jana kwa hasira nikaamua kuchepuka, mwanzo nilikua na amani lakini sasa hivi sina amani kwani naona kama mume wangu haumii. Yeye anachepuka mimi najua nateseka lakini yeye hajui kama mimi nateseka.

Tumeshaitishwa vikao mpaka wametuchoka, nataka kumuumiza mume wangu, nataka ajue uchungu ninaoupitia, nataka kumuonyesha kuwa nina mwanaume mwingine, nashindwa nifanyeje, niache meseji au nipige picha nikiwa na mwanaume mwingine ili aone.

Nataka aumie kama ninavyoumia.
Piga magoti utubie dhambi yako ya uzinzi na utubu kwa ajili yake....

Sali Sana, tena sanaaaa kama bado unahitaji hiyo ndoa.

Hicho kisasi unachokitamani kinaweza kugeuka anguko lenu wote.
 
Back
Top Bottom