Nifanye nini? Ndoa ina miezi 10, mke wangu kabadili dini kaolewa na mwanaume mwingine

Tajiri wa matajiri

Senior Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
166
Reaction score
649
Niliunganishwa na huyu mke wangu na shangazi yangu. Kipindi hicho nilikuwa nimetoka masomoni Uingereza, na kwa kuwa nilitoka huko nikiwa na kazi tayari, hivyo nilikuwa nishajipanga kimaisha na mambo yalikuwa mazuri. Sikupanga kuoa kwa kipindi hicho, lakini kama unavyojua familia zetu, ukiwa na miaka 36, una PhD na kipato kizuri basi kelele ni kuoa.

Kipindi naondoka Tanzania nilikuwa na mchumba, ila kutokana na umbali, alishindwa kuvumilia miaka 3 hivyo nilirudi nikiwa sina mtu. Shangazi yangu aliniunganisha na huyu binti akiniambia ni mtoto wa rafiki yake hivyo anamjua na anajua familia yake vizuri.

Sikupenda mambo ya kuunganishwa lakini baada ya kumuona basi nilichanganyikiwa na mapenzi yakaanza. Kusema kweli tulikuwa vizuri, tunazungumza, tunacheka na ndani ya miezi 6 tulishafika mashabahuni na kuapa mpaka ki*fo kitutenganishe.

Sikujua chochote kuhusu mahusiano yake ya nyuma mpaka wiki mbili baada ya ndoa, baada ya kuwa karibu sana na mke wangu ndipo nikagundua kuwa ile furaha aliyokuwa ananionyesha ilikuwa ni ya kuigiza. Kulikuwa na namba fulani alikuwa anachati nayo mara kwa mara. Sikutaka kumfuatilia ila niliona ni kama ni mama yake, lakini kuna siku meseji za mapenzi zikaingia na nikajiuliza, anachati mapenzi na mama yake?

Basi nikaamua kufuatilia, na kwa ujuzi wangu haikuchukua muda nikajua alikuwa anawasiliana na X wake. Hapo ndipo niligundua kuwa mke wangu kabla yangu alikuwa na mchumba kwa miaka kama 7 hivi, walipendana sana, lakini alipompeleka kwao, mama yake alimkataa kwa sababu ya dini.

Waligoma kupokea mahari na mwaka mzima walikuwa wakimsumbua, binti alikuja kukubali kuachika baada ya kijana kuamua kuoa mwanamke mwingine. Ila bado waliendelea kuwasiliana, lakini binti hakutaka kuniambia akiamini kuwa ningemuacha. Ukweli ni kuwa ningemuacha lakini tayari tumeshaingia kwenye ndoa, tena ya Kikatoliki, utatoka vipi?

Basi tulizungumza, akaomba msamaha na kuniambia hawatawasiliana tena. Lakini baada ya hapo ndipo ikawa shida tena ndani, kila kitu ni kugombana, kuninunia bila sababu. Alikuwa ananifanyia vituko mpaka nikagundua kuwa anatafuta sababu za kugombana ili tu tukinuniana awe bize kuchati na mwanaume wake. Ilifikia kipindi hali ilinichosha, nikamtafuta yule mwanaume kumuomba amuachie mke wangu, si ana mke wake bwana!

Hapo ndipo niliharibu, maana alinitukana sana, akanisema mambo mengi, lakini kubwa lililoniumiza ni kuniambia kuwa mke wangu ni mjamzito na mimba ni yake. Sikuamini kwani nikikumbuka juzi mke wangu ndiye aliyeniambia nimnunulie pedi, ujauzito unatoka wapi? Lakini niliporudi nyumbani kuongea na mke wangu, akaniambia ni kweli ana ujauzito wa miezi 3, lakini mimba ni yangu kwani hajawahi kulala na huyo mwanaume.

Nilipomuuliza kwa nini hukunambia, aliniambia sikujua, kwani bado nilikua naona siku zangu. Nilivyokuwa mjinga niliamini, ila mwezi uliopita mke wangu aliniaga anaenda kwao kujifungua.

Basi tukaongea vizuri nilitaka kumpeleka akaniambia Hapana nitaenda mwenyewe. Sasa juzi mama yake akanipigia simu kuniuliza kwa nini sijampeleka mke wangu kujifungua wakati tulishakubaliana hivyo. Nikamwambia mbona kaniambia anakuja huko! Basi katika kutafuta na kuhangaika, naambiwa mke wangu kaenda ukweni, yaani kwa huyu mwanaume, na huko ndiyo ameenda kujifungua na amebadili dini wamefunga ndoa ya Kiislamu.

Nilimtafuta, akaniambia ni kweli. Akasema nimeamua nisidanganye tena, huyu mtoto si wako, ni wa huyu mwanaume wangu. Nimeamua kubadili dini ili kufuata moyo wangu. Wewe ni mwanaume mzuri sana, ulinipokea na kunikubali na machungu yangu, naamini Mungu atakubariki na mwanamke mwingine.

Lakini mimi sasa ni mke wa mtu, endelea na maisha yako! Kwa kweli sijui nifanye nini, nimechanganyikiwa hata kutoka ndani nashindwa. Sijaweza kumuambia mtu yeyote hata wazazi wangu, siwezi kuongea nao
 
Mleta mada,kwanini akili yangu inaniambia wewe haukusoma Uingereza?

Yaani hata mada sijaimaliza lakini kichwani kunalia alarm kwamba huyu mleta mada hiyo kwenda kusoma nje ameiweka tu kama kibwagizo asionekane hamnazo saana!!!
 
Pole kwa matatizo mkuu naamini hii story ni ya kweli na yamekukuta wewe.

Biblia inasema mke haachwi ila kwa zinaa tu. Kwa hiyo una kila sababu ya kumuacha na hamna kitu atafanya.

1. Shirikisha mshenga wako jambo hili na ataita pande zote mbili kumaliza hiyo ndoa.
2. Shirikisha viongozi wa kanisa lako ilipofunga ndoa uvunje hiyo ndoa.
3. Shirikisha wazazi wako.
4. Tafuta namna ya kusahau hilo jambo. Shiriki mazoezi, kuwa busy na kazi, nenda vacation n.k

NB: Hakikisha juu chini ndoa inavunjwa na mahakama na uwe una ushahidi.

Wazazi wake wanajua wanakuchezea shere tu.
 
Niliunganishwa na huyu mke wangu na shangazi yangu. Kipindi hicho nilikuwa nimetoka masomoni Uingereza, na kwa kuwa nilitoka huko nikiwa na kazi tayari, hivyo nilikuwa nishajipanga kimaisha na mambo yalikuwa mazuri. Sikupanga kuoa kwa kipindi hicho, lakini kama unavyojua familia zetu, ukiwa na miaka 36, una PhD na kipato kizuri basi kelele ni kuoa.

Kipindi naondoka Tanzania nilikuwa na mchumba, ila kutokana na umbali, alishindwa kuvumilia miaka 3 hivyo nilirudi nikiwa sina mtu. Shangazi yangu aliniunganisha na huyu binti akiniambia ni mtoto wa rafiki yake hivyo anamjua na anajua familia yake vizuri.

Sikupenda mambo ya kuunganishwa lakini baada ya kumuona basi nilichanganyikiwa na mapenzi yakaanza. Kusema kweli tulikuwa vizuri, tunazungumza, tunacheka na ndani ya miezi 6 tulishafika mashabahuni na kuapa mpaka ki*fo kitutenganishe.

Sikujua chochote kuhusu mahusiano yake ya nyuma mpaka wiki mbili baada ya ndoa, baada ya kuwa karibu sana na mke wangu ndipo nikagundua kuwa ile furaha aliyokuwa ananionyesha ilikuwa ni ya kuigiza. Kulikuwa na namba fulani alikuwa anachati nayo mara kwa mara. Sikutaka kumfuatilia ila niliona ni kama ni mama yake, lakini kuna siku meseji za mapenzi zikaingia na nikajiuliza, anachati mapenzi na mama yake?

Basi nikaamua kufuatilia, na kwa ujuzi wangu haikuchukua muda nikajua alikuwa anawasiliana na X wake. Hapo ndipo niligundua kuwa mke wangu kabla yangu alikuwa na mchumba kwa miaka kama 7 hivi, walipendana sana, lakini alipompeleka kwao, mama yake alimkataa kwa sababu ya dini.

Waligoma kupokea mahari na mwaka mzima walikuwa wakimsumbua, binti alikuja kukubali kuachika baada ya kijana kuamua kuoa mwanamke mwingine. Ila bado waliendelea kuwasiliana, lakini binti hakutaka kuniambia akiamini kuwa ningemuacha. Ukweli ni kuwa ningemuacha lakini tayari tumeshaingia kwenye ndoa, tena ya Kikatoliki, utatoka vipi?

Basi tulizungumza, akaomba msamaha na kuniambia hawatawasiliana tena. Lakini baada ya hapo ndipo ikawa shida tena ndani, kila kitu ni kugombana, kuninunia bila sababu. Alikuwa ananifanyia vituko mpaka nikagundua kuwa anatafuta sababu za kugombana ili tu tukinuniana awe bize kuchati na mwanaume wake. Ilifikia kipindi hali ilinichosha, nikamtafuta yule mwanaume kumuomba amuachie mke wangu, si ana mke wake bwana!

Hapo ndipo niliharibu, maana alinitukana sana, akanisema mambo mengi, lakini kubwa lililoniumiza ni kuniambia kuwa mke wangu ni mjamzito na mimba ni yake. Sikuamini kwani nikikumbuka juzi mke wangu ndiye aliyeniambia nimnunulie pedi, ujauzito unatoka wapi? Lakini niliporudi nyumbani kuongea na mke wangu, akaniambia ni kweli ana ujauzito wa miezi 3, lakini mimba ni yangu kwani hajawahi kulala na huyo mwanaume.

Nilipomuuliza kwa nini hukunambia, aliniambia sikujua, kwani bado nilikua naona siku zangu. Nilivyokuwa mjinga niliamini, ila mwezi uliopita mke wangu aliniaga anaenda kwao kujifungua.

Basi tukaongea vizuri nilitaka kumpeleka akaniambia Hapana nitaenda mwenyewe. Sasa juzi mama yake akanipigia simu kuniuliza kwa nini sijampeleka mke wangu kujifungua wakati tulishakubaliana hivyo. Nikamwambia mbona kaniambia anakuja huko! Basi katika kutafuta na kuhangaika, naambiwa mke wangu kaenda ukweni, yaani kwa huyu mwanaume, na huko ndiyo ameenda kujifungua na amebadili dini wamefunga ndoa ya Kiislamu.

Nilimtafuta, akaniambia ni kweli. Akasema nimeamua nisidanganye tena, huyu mtoto si wako, ni wa huyu mwanaume wangu. Nimeamua kubadili dini ili kufuata moyo wangu. Wewe ni mwanaume mzuri sana, ulinipokea na kunikubali na machungu yangu, naamini Mungu atakubariki na mwanamke mwingine.

Lakini mimi sasa ni mke wa mtu, endelea na maisha yako! Kwa kweli sijui nifanye nini, nimechanganyikiwa hata kutoka ndani nashindwa. Sijaweza kumuambia mtu yeyote hata wazazi wangu, siwezi kuongea nao
Iyo PHD ulisomea nini?
Mbona akili za darasa la 5 hizi
 
Kabisa
images%20(11).jpg
 
We jamaa acha nikutukane tuu pamoja na PHD yako lakini wewe ni mpumbavu samahani kwa hilo lakini ulipaswa kuachana na huyo shetani ulivyo mgundua kwa mara kwanza kujikuta Koffi Annan kwamba unaweza kusawazisha mambo ndio mara zote hutokea hivyo

kuendelea kumuwaza na kushindwa kufanya maisha yako ndio upumbavu zaidi achana nae fanya maisha yako
 
Back
Top Bottom