Nifanye nini? Ndoa ina miezi 10, mke wangu kabadili dini kaolewa na mwanaume mwingine

Iyo PHD ulisomea nini?
Mbona akili za darasa la 5 hizi

Achana na mdudu anaitwa mapenzi. Na hasa uoneshe kumpenda kuliko maelezo, atafanya kila lililo mkononi mwake. Werevu wengi sana hata kwenye vitabu vitakatifu waliangushwa na kitu mapenzi
 
Wahenga walisema mapenzi upofu, mapenzi ni zaidi ya elimu ya darasani. Hata mwenza akiwa sawa kabisa, shetani atapanda mbegu tu.
Mimi nakushauri kitu kimoja, badilisha kabisa aina ya maisha ili kumbukumbu zake zife/ Hapa hakuna siri tena, washiirikishe viongozi wa kanisa, wazazi na ndugu zako na mtakaa na kupata mustakabali mzuri kabisa wa maisha. Mshukuru sana Mungu amekuondolea hii kero mapema vinginevyo ungejuta sana mbele maishani
 
Dah inabidi uwe jasiri na ujikaze umsahau hamna namna...
 
Kubalian halo, songq mbele pia amekupa nafasi ya kukumbatia mtu mpya (imagine raga ya kukumbatia damu mpya).
 
Mamwanamke yamejaa huko mtaani,unalilia hilo malaya?
 
Njoo tuungane mimi na wewe tunashida zinazofanana .
 
Mkuu ndia ya kikristo haivunjwi mtaani wala kwa mihemko. Afuate process.
 
Mm sina mengi

Kamati imeshaongea sana msioe
 
Nyie ndo mnafanya elimu ionekane haina maana,msomi mwenye pHD eti hujui kama.mkeo mjamzito,hufatilii bleed zake kila mwezi?
 
Labda PhD ya Hemed😅
😂 hemed huyu huyu Felnando Papi, Karitolinasto Armando Felila, Morientesi, Moravido, Marcelo Kuchito Papa Gichito, Gustavo, Ole Sabaya Hamza Mwamposa Kapumbu, aaih Kardashiani. Wananiita Pumbuyo, Punyeto, Papusi a.k.a Mguu wa mtoto wa miaka saba mpaka nane.
 
Huyo jamaa anaishi na mke wa mtu hapo ni kesi ya ugoni tu inahusika kukiwa na fidia endapo ukitaka nafikiri.

Ni ngumu kulichukua ila acha aende. Duniani tunapata majeraha yanatuachia makovo ila maisha yanasonga mbele. Jambo la msingi usichukue hatua ya kujidhuru kwa sababu ya mwanamke. Hakuna aliye wa thamani zaidi yako. Yupo mwanamke anakusubiri.
 
Kosa lilianza pale ulipokubali kutafutiwa mke.

USHAURI;
Hakikisha ndoa hyo inavunjwa na mahakama, bila kujali unampenda kiasi gani tafadhari usithubutu kuendelea na hyo ndoa, kwa gaharama yoyote vunja hyo ndoa

Usipepese macho katika kuanza safari mpya, maumivu ya mapenzi huwa yanauma sana lkn yanazoeleka. Nakuhakikishia utazoea na msiaha yataendelea

Baada ya kuacha naye ni vema usikimbilie kutafuta mtu mwingine, mara nyingi maamuzi ya kutafuta mwenza ukiwa na maumivu ya kuachwa huwa sio sahihi, unaweza kumchukua mtu ili kutuliza maumivu lkn baada ya kutulia unagundua ulifanya makosa. Tulia, hata ukioa na miaka 45 sio dhambi na uwambie ndugu kabisa wakae mbali katika hilo utaamua mwenyewe kwa wakati wako.

Take it itakusaidia
 
Kama sio chai pole sana, pole nyingi kwa kweli.
Kama nyie wenye PHD mnakimbiwa kizembe namna hio sisi wa la saba sijui itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…