Nifanye nini niepuke kivuli cha ex husband asiyekubali kuachana?

Lagertha

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2023
Posts
212
Reaction score
694
Salaam WanaJF,

Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana — mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF – kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.

Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.

Narudi kwenye mada kuu...

Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu – sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.

Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom – japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.

Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.

Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika — nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".

Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.

Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana – zote mbili – lakini bado habadiliki.

Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu — nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?

Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
 
Alipokupa talaka mlikwenda kuithibitisha mahakamani, au mliishia hapohapo BAKWATA?

Kama mlikwenda mahakamani, kuna namna unaweza kufungua maombi juu ya amri hiyo ikiwa ni pamoja na kuwekwa umbali wa yeye kukaribiana nawe.

Ila kama mliishia BAKWATA, sasa itabidi mwende mahakamani kukamilisha talaka na hapo utaweza kuomba hizo amri za umbali.

Njia ya haraka ni kutoa taarifa polisi kuwa anakubughudhi, na pia unaweza fungua kesi ya madai kwa kukupotezea wateja na kukuingiza hasara kwenye biashara zako.
 


Mwishowe tutakuzika, Fanya uwezavyo uhame na asiweze kukufukia Maisha yake yote.

Ila hapo kumpiga mwanaume aliyekuchumbia mpaka akakuacha ni kama chai vile???!!!

Pia ninahisi ni kweli ulikuwa humtaki jamaa wakati Hali yake ya uchumi ni mbaya, kwa mwanaume hiyo inauma.
 
Kudili na huyo fala kistaarabu ni mpaka yeye tu aamue kuwa mstaarabu,

Kuliko kusubiri eti ustaarabu umjie kuna njia zingine za kihuni zipo na ndio unatakiwa uzitumie, inabidi tu ukubali kuwa... amani inaweza tafutwa kwa kutumia vita.

Tafuta mume muhuni anayeweza deal perpendicular na huyo fala, au kodi wahuni wamshugulikie ili aache ufala huo.
 
Hatimaye sasa umekutana na mme sahihi .

Zama PM chap weka namba hapa binti ,mimi ndiye dawa ya wanaume wajinga kama hako kaex kako .

Sijisifii ila ngumi za kupiga niko sawa nina mkanda mweusi wa karate ,kuhusu sheria hapa ndiyo mahali pake .

Ila pia hela si haba si nimeajiriwa bwana ,nakuambia kuwa huyo mjinga atajuta kukujua nitapiga alafu niweke ndani hata mwaka .

Nathubutu kusema suluhu ya shida zako ni mimi kwakuwa naona umeteseka sana .

Anyway zifuatzo ni sifa zangu mwanaume shababi hapa .

Mfupi kiasi
Nina tumbo kubwa ila lenye kuleta heshima kwa jamii ya watu waliostaarabika .

Ni mshari na mgovi haswa kwa wakorofi kama hako kaex kako .

Siko tayari kushuhudia maonezi yoyote .

Nimeajiriwa na serikali tukufu ya Tanzania .
Nina usafiri wangu mzuri mno (corolla ) nzuri mkoa mzima hakuna mwenye nayo kama hii .

Si bahili haswa nikipenda kama hivi .
Jitahidi kuwahi Pm kwangu maana kuna wanawake wataanza kunisumbua kwa wasifu wangu mkubwa wa namna hii .

Asante ,karibu nikutetee bibiye .
 
Afuate ushauri wako,asitafute Amani wakati wa vita,vita ni vita Mura😬😬😬😬
 
Ewaaaaahhhh!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…