The mission 2017
JF-Expert Member
- Aug 14, 2017
- 6,498
- 14,946
Kuna kitu hakiko sawa kwenye maisha yako.
Unakaa wapi huko, ambapo kila ukifanya x wako anapata taatifa?
Unakaa wapi huko, ambapo kila ukifanya x wako anapata taatifa?
Hii taarifa ilibidi uwape polisi chukua RB ...AITWE polisi kuwa lolote baya likitoke yeye wa kwanzaSalaam wana JF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta tatizo langu zito lilokua linanikabili, kwanza niwapongeze mlinisaidia sana, mlinipa moyo na shauri mbalimbali, nilikua nimekata tamaa ya kuishi, nilijiona sina thamani tena lakini thread moja tu iligeuza maisha yangu yote, nilipata nguvu na kusimama tena hadi leo hii,
Nawashukuru sana wanaJF kuanzia viongozi hadi wanachama, wito wangu msiubeze uzi wa mtu anayeomba msaada hamuwezi jua wakati huo amefikia stage gani, sio kila mtu ana ndugu, marafiki au majirani wa kushea nao yanayomsibu,
********
Narudi kwenye mada kuu,
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kua jehanam, alikataa katakata kunipa talaka, nilichoka kuishi nikiwa sijui hatma yangu, sijijui ni mke wa mtu au msela maana mwanaume aliondoka na kuniacha nikiwa na mtoto wake tumboni na hata alipozaliwa bado hakunihudumia kwa lolote, nilivumilia nikachoka nikamwambia anipe talaka yangu ili kila mtu aendelee kuishi kwa amani zake, nilikubali kua rasmi a single mom kundi ambalo linanyanyaswa na kupewa dhihaka kila kukicha na wanaume wa kiTanzania, yule mwanaume aligoma kuniacha na hapo hapo hakua anatoa msaada wowote, baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section) nikaamua kwenda BAKWATA kuidai talaka yangu alipoitwa mara kadhaa hakawa haendi alifatiliwa sana ikabidi aje, akadai yeye bado ananipenda ila anaendelea kujitafuta akipata atanirejea, ilikua ni sababu isiyo na mashiko nikasema basi najivua mimi hiyo ndoa na kurudisha mahari yake, hapo ndipo alipokubali kutoa talaka baada ya hapo ndio mikasa yake ilipoanza, akageuka stalker, kila sehemu nilipo na yeye yupo......
Nilifungua duka alikua anakuja dukani kila siku anakaa pembeni ya duka kuna mtu anaduka la chakula, akawa anaenda hapo anaagiza vinywaji, mteja wa kiume akisimama sana dukani kwangu anakuja atajifanya na yeye ni mnunuzi atagombana nae, kero zilizidi hadi wateja wakapungua, na mimi nikafunga duka, nikaanza biashara nyingine hali ni ile ile, nikapata mwanaume akaja kunichumbia sijui alijuaje akamtafuta huyo mwanaume akampiga sana na kumwambia akae mbali na mke wake, mwanaume akapotea, nahisi hata simu yangu ameihack, sina raha na huyu mwanaume, sijui ananitaka kitu gani, sijui ana lengo gani na mimi, yaan muda wa kunifatilia anao ila muda wa kutafuta hela amuhudumie mtoto wake hana, amekua mwiba kwangu, amekua akiniambia maneno ya kutisha nimuonavyo ni mtu ambaye yupo tayari hata kuniua lakini nashangaa sie mimi niliyemuacha na kumtelekeza kwanini awe na chuki kali na mimi? nilimbembeleza sana arudi nyumbani akasema hawezi leo nime move on anataka kuniharibia maisha, familia za pande zote wameshaongea nae sana anaahidi ataacha lakini wembe ni ule ule, naombeni ushauri mtu kama huyu naweza kumfanyaje aache kunisumbua?
Aende polisi.Kudili na huyo fala kistaarabu ni mpaka yeye tu aamue kuwa mstaarabu,
Kuliko kusubiri eti ustaarabu umjie kuna njia zingine za kihuni zipo na ndio unatakiwa uzitumie, inabidi tu ukubali kuwa... amani inaweza tafutwa kwa kutumia vita.
Tafuta mume muhuni anayeweza deal perpendicular na huyo fala, au kodi wahuni wamshugulikie ili aache ufala huo.
Haupo serious wewe, na anakujua udhaifu wako hivyo atazidi kukuchezea akili na kukuharibia.Salaam WanaJF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana — mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF – kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.
Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.
Narudi kwenye mada kuu...
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu – sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.
Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom – japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.
Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.
Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika — nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".
Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.
Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana – zote mbili – lakini bado habadiliki.
Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu — nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?
Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
Asithubutu kufanya hivyo.Sijui kwanini Tz restraining order huwa hazina mashiko.
Ukijichukulia kuwa ni muhanga na dhaifu kwake, daima atakupanda kichwani na kukufanya atakavyo.
Huyo jamaa yako ni bully, muonevu. Njia pekee ya kumdhibiti mtu kama huyo ni kumkabili. Jitoe ufahamu umjazie watu kila pale anapokuandama. Ukimdhalilisha mara mbili tatu, ataondoka na asirudi tena.
Najua ni ngumu kumchagua wa kumpenda, ila ifikie wakati uchague mwanaume anaejimudu kiubavu kuingia nae kwenye mahusiano. Maana kumpenda mtu asieweza hata kujitetea kiasi cha kudundwa kizembe hapo kuna walakini pia.
Kila la heri mama.
Wenzio wamekung'untwa hadi wakaomba poo halafu wewe unataka ulianzishe?Nikubalie mimi nikuoe basi hatakusumbua tena
Pole kwa kuangukia katika ndoa ya mwanaume asiyejitambua.Salaam WanaJF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana — mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF – kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.
Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.
Narudi kwenye mada kuu...
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu – sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.
Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom – japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.
Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.
Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika — nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".
Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.
Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana – zote mbili – lakini bado habadiliki.
Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu — nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?
Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
Hii sheria ya kukaa mbali kwa mita kadhaa huku kwetu inatendeka kweli? Walai naitaka maana nimechoka sanaKusanya ushahid wa anayokutendea ikibid aliowahi kuwadunda au kuwapiga mikwa waje watestfy mahakama itamuamuru akae maelfu ya kilometa za mraba mbali na maisha yako