Nifanye nini niepuke kivuli cha ex husband asiyekubali kuachana?

Nifanye nini niepuke kivuli cha ex husband asiyekubali kuachana?

Na umejuaje navaa nikhabu na pia ni mtoto wa mwisho😄
Nilijua kwa sababu umeelezea story yako upande wako tu. Hata huko kukushauri inakuwa vigumu kwasababu hatujamsikia jamaa anasemaje.
Lakini pia inaonekana unaamini TALAKA ni jambo rahisi sana na nisuluhisho la kila changamoto iliyopo mbele yako kwenye ndoa. Hii usipojipanga itakusumbua sana.
Hakuna mwanaume mjinga eti amwache tu mke wake aondoke hakuna
 
Pole kwa kuangukia katika ndoa ya mwanaume asiyejitambua.

Ndoa ni mkataba wa hiari kati ya mume na mke kuishi pamoja au siyo?

Ndoa hailazimishwi, mmoja akitaka kuivunja, inavunjika na kila upande kupata haki yake.

Huyo X-mmeo ni kati ya wanaume wapumbaf wanaochukulia mke ni kama bidhaa ya kumiliki na kuhodhi na si muunganiko wa wapendanao wenye haki sawa mbele za Mungu na mbele za sheria.

Cha kufanya, anzisha mahusiano mengine ili aingie kwenye mfumo kama ataendelea kukuzoea.

Akiingila uhuru wako tu, tengeneza ushahidi uliokamilika, buruza mahakamani kama unaua nyani bila kumuangalia usoni, pia dai talaka yako.

Tatizo nimeliona katika mada yako ni kwamba, unamlegezea sana huyo bazazi.
Talaka uliyoidai, uliidai kwa nani na kwa njia gani, mbona haujatupatia mwendelezo wake?

Huyo unampetpet kama mume au ndugu, huyo ni adui yako, kaza fuvu ili kumuondoa kabisa katika mzunguko wa maisha yako na kubakia na uhuru wako.
Talaka nilienda kuidai Bakwata, nilikua tayari kujivua na kumrejeshea mahari yake hiyo ndio ikawa sababu akakubali kuitoa yeye,
Ni kweli mwanzo nilikua nampeti peti arejee tulee mtoto lakini hakurudi baada ya talaka ndio amegeuka na kuanza kuniharibia maisha yangu, ajabu mtoto wake hana time nae yeye ana deal na mimi tu
 
Nilijua kwa sababu umeelezea story yako upande wako tu. Hata huko kukushauri inakuwa vigumu kwasababu hatujamsikia jamaa anasemaje.
Lakini pia inaonekana unaamini TALAKA ni jambo rahisi sana na nisuluhisho la kila changamoto iliyopo mbele yako kwenye ndoa. Hii usipojipanga itakusumbua sana.
Hakuna mwanaume mjinga eti amwache tu mke wake aondoke hakuna
Uzi niliowahi kuuleta huu hapa, mie sina nongwa nae kwa haki kabisa nilijaribu kwa upande wangu ila alizidi kunisukumia mbali,

Thread 'Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana' Moyo wangu unaungua, Akili inaharibika, Mwili unakonda, Mapenzi yanatesa sana
 
Alipokupa talaka mlikwenda kuithibitisha mahakamani, au mliishia hapohapo BAKWATA?

Kama mlikwenda mahakamani, kuna namna unaweza kufungua maombi juu ya amri hiyo ikiwa ni pamoja na kuwekwa umbali wa yeye kukaribiana nawe.

Ila kama mliishia BAKWATA, sasa itabidi mwende mahakamani kukamilisha talaka na hapo utaweza kuomba hizo amri za umbali.

Njia ya haraka ni kuyoa taarifa polisi kuwa anakubughudhi, na pia unaweza fungua kesi ya madai kwa kukupotezea wateja na kukuingiza hasara kwenye biashara zako.
Hapana talaka hatukuithibitisha mahakamani, umenipa wazo jipya itabidi niifatilie hii,
Shukrani sana
 
Hatimaye sasa umekutana na mme sahihi .

Zama PM chap weka namba hapa binti ,mimi ndiye dawa ya wanaume wajinga kama hako kaex kako .

Sijisifii ila ngumi za kupiga niko sawa nina mkanda mweusi wa karate ,kuhusu sheria hapa ndiyo mahali pake .

Ila pia hela si haba si nimeajiriwa bwana ,nakuambia kuwa huyo mjinga atajuta kukujua nitapiga alafu niweke ndani hata mwaka .

Nathubutu kusema suluhu ya shida zako ni mimi kwakuwa naona umeteseka sana .

Anyway zifuatzo ni sifa zangu mwanaume shababi hapa .

Mfupi kiasi
Nina tumbo kubwa ila lenye kuleta heshima kwa jamii ya watu waliostaarabika .

Ni mshari na mgovi haswa kwa wakorofi kama hako kaex kako .

Siko tayari kushuhudia maonezi yoyote .

Nimeajiriwa na serikali tukufu ya Tanzania .
Nina usafiri wangu mzuri mno (corolla ) nzuri mkoa mzima hakuna mwenye nayo kama hii .

Si bahili haswa nikipenda kama hivi .
Jitahidi kuwahi Pm kwangu maana kuna wanawake wataanza kunisumbua kwa wasifu wangu mkubwa wa namna hii .

Asante ,karibu nikutetee bibiye .
Kwa hivyo nianze tu kusema "mume ninae na ninatamba nae" 😄
 
Mwishowe tutakuzika, Fanya uwezavyo uhame na asiweze kukufukia Maisha yake yote.

Ila hapo kumpiga mwanaume aliyekuchumbia mpaka akakuacha ni kama chai vile???!!!

Pia ninahisi ni kweli ulikuwa humtaki jamaa wakati Hali yake ya uchumi ni mbaya, kwa mwanaume hiyo inauma.
Wallah sio chai, ilikua fujo kila siku yaan tafrani na baada ya huo ugomvi mchumba akasema basi inatosha, hawezi kua na amani na mimi ilhali huyo jamaa hajataka kuniacha, akasamehe hadi mahari
 
Amekuwa kama wale wa kwenye movie za kihindi
Mkorofi akiona mwanaume anamahusiano na ww ni kichapo😎
 
Amekuwa kama wale wa kwenye movie za kihindi
Mkorofi akiona mwanaume anamahusiano na ww ni kichapo😎
72D2E4AC-353E-4DC4-AEB0-B912E766E817.jpeg
 
Hapana talaka hatukuithibitisha mahakamani, umenipa wazo jipya itabidi niifatilie hii,
Shukrani sana
Hapo kisheria bado ni mumeo. Nenda mahakamani kakamilishe jambo lako. Ukitaka msaada zaidi wa kisheria nicheki kwa 0713368153.
 
Jitahidi utoe taarifa polisi, talaka yako kama ni ya bakwata enda mahakamani ili sasa sheria ikusaidie na kuweka mipaka juu yenu, itasidia zaidi nakushauri hama mkoa ulipo kama unaweza, kutana na watu wapya wasiokujua kabisaaa maana unavoanzisha jambo jipya hao hao ndio wanaompa ramani na taarifa zako. Mwisho kabisa ukishahama badili namba zako za simu
 
Back
Top Bottom