Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,029
Binafsi nakushauri yafuatayo;Salaam WanaJF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana — mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF – kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.
Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.
Narudi kwenye mada kuu...
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu – sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.
Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom – japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.
Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.
Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika — nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".
Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.
Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana – zote mbili – lakini bado habadiliki.
Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu — nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?
Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
1. Biashara unazofungua, usikae wewe mwenyewe kuzifanya. Weka mtu/watu unaowaamini, mpaka hapo mambo yatakapotengamaa. Hii hasa kama sehemu mliyokuwa manishi ni eneo hilo hilo unalofungulia biashara
2. Kwa vitisho na vipigo anavyowapa wanakutaka, nenda polisi katoe taarifa. Ataitwa na kupewa ultimatum
3. HAMA MJI. KAMA MNAISHI MBEYA, WE SEPA ZENJI KIMYAKIMYA. KAMA MPO DAR, WAHI ZAKO MBINGA HUKO KIMYA KAANZE MAISHA MAPYA