Nifanye nini niepuke kivuli cha ex husband asiyekubali kuachana?

Nifanye nini niepuke kivuli cha ex husband asiyekubali kuachana?

Kwanini msikae mkaelewana badala ya kuwaza kuachanaa kampeti pet huyo mmeo akili yake itulie Sio unakimbia tatizo
 
Jitahidi utoe taarifa polisi, talaka yako kama ni ya bakwata enda mahakamani ili sasa sheria ikusaidie na kuweka mipaka juu yenu, itasidia zaidi nakushauri hama mkoa ulipo kama unaweza kutana na watu wapya wasiokujua kabisaaa maana unavoanzisha jambo jipya hao hao ndio wanaompa ramani na taarifa zako. Mwisho kabisa ukishahama badili namba zako za simu
Shukrani sana, hili nimelizingatia la kuhama mkoa
 
Salaam WanaJF,

Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana — mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF – kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.

Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.

Narudi kwenye mada kuu...

Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu – sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.

Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom – japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.

Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.

Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika — nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".

Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.

Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana – zote mbili – lakini bado habadiliki.

Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu — nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?

Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
Pole sana. Aisee bila kupepesa macho nikuambie huyo jamaa yako ni mtu hatari sana. Usicheke naye na wala usijifanye mnyonge. Wanaume wa aina hiyo hawakuwii kuua au kufanya jambo baya sana. Anaweza hata kukodi watu wakakumwagia acid ili kukukomoa. Tumia njia za kisheria na iambie familia yako ikusaidie.
 
Wewe hauna kaka au baba au mjomba? Yani huna ndugu mwanaume wa kukusaidia?

Huyo angekutana na kaka yangu mmoja kichaa hivi angenyooshwa
 
Talaka nilienda kuidai Bakwata, nilikua tayari kujivua na kumrejeshea mahari yake hiyo ndio ikawa sababu akakubali kuitoa yeye,
Ni kweli mwanzo nilikua nampeti peti arejee tulee mtoto lakini hakurudi baada ya talaka ndio amegeuka na kuanza kuniharibia maisha yangu, ajabu mtoto wake hana time nae yeye ana deal na mimi tu
Mshitaki kwa jinai mahakamani.

Kikubwa, andaa mazingira ya kupata ushahidi wa vurugu zake unaoweza kumtia hatiani, kisha buruza mahakamani.

Talaka ushapewa, kitu gani kinakufanya uwe mpole na usimshitaki?

Tatizo lenu kina mama, yawezakuwa anakulala kisiri, sasa ashakufanya hawara yake, maana ni ngumu sana mtu kumchezea mtalaka wake kwa vitendo kama anavyokufanyia kisha umlegezee!

atacheza sana na saikolojia yako usipokomaa!
 
Options mbili
  • Hama eneo/mkoa huo ukaanze kwingine upya.
  • Nenda kwa vyombo vya ulinzi/sheria wakupe mwongozo, akikaa ndani wiki moja atakuacha uendelee na phase nyingine ya maisha.
 
Tatizo lenu kina mama, yawezakuwa anakulala kisiri, sasa ashakufanya hawara yake, maana ni ngumu sana mtu kumchezea mtalaka wake kwa vitendo kama anavyokufanyia kisha umlegezee!

atacheza sana na saikolojia yako usipokomaa!
Umehukumu vibaya sana, futa hiyo kauli yako, ingekua bado tunatembea ningekuja kuomba msaada/ushauri? kama bado tunaendeleza mahusiano unadhani angefanya hayo anayoyafanya? si tungekua happy tunalea zetu mtoto wetu,

Umenikera sana laiti ungejua....!?
 
Pole sana. Aisee bila kupepesa macho nikuambie huyo jamaa yako ni mtu hatari sana. Usicheke naye na wala usijifanye mnyonge. Wanaume wa aina hiyo hawakuwii kuua au kufanya jambo baya sana. Anaweza hata kukodi watu wakakumwagia acid ili kukukomoa. Tumia njia za kisheria na iambie familia yako ikusaidie.
Ahsante sana,
Ni kweli amekua mkatili na ndio kinachonitisha, kwa hatua alofika namuona kabisa yupo tayari kufanya lolote kuniangamiza lakini nashangaa mie sie adui wake, sijui kwanini amenichukia namna hii
 
Umehukumu vibaya sana, futa hiyo kauli yako, ingekua bado tunatembea ningekuja kuomba msaada/ushauri? kama bado tunaendeleza mahusiano unadhani angefanya hayo anayoyafanya? si tungekua happy tunalea zetu mtoto wetu,

Umenikera sana laiti ungejua....!?
Pole, nisamemee bure mkuu.

Nimeingiza hicho kionjo kutokana na uzoefu.

Kuna jirani yangu hapa, walitalikiana na jamaa, vurugu zikawa haziishi, kumbe wanalalana tena!

Kwa hiyo mkuu, si ajabu sana, ni matendo yanayofanywa na jamii, kwa hiyo kama wewe hufanyiiv'o basi sawa, zuia jamaa asikuchezee akili zako.
 
Wewe mleta uzi nadhani kuna kaupumbavu fulani umekuwa ukikafanya kanakomfanya huyo mumeo afanye anayoyafanya. Dada, mwanamke aliyechoka na manyanyaso ya mumewe huwa akisema inatosha, sisi wanaume wenyewe huwa tunapisha njia. Endelea kumfurahia mpaka siku akutie chongo ndio utazinduka
 
Shirki ndo nini

Umeuliza hivi ukimaanisha hujui nini maana ya shirki au umeuliza hivyo kwa kejeli na kuidogosha dhambi hiyo kubwa kuliko dhambi zote ambayo ikifanywa inaharibu matendo mema na Allah hamsamehi aliyeifanya (akifa bila ya kutubia)?

Ninamuomba Allah anikinge kutokamana na dhambi hiyo mbaya kabisa na aniweke mbali nayo, Aamiin

Ninamuomba Allah aniepushe na shirki na ukafiri na maasi mengine mimi na wewe na ndugu yetu huyo, na atuongoze sisi na wewe katika njia iliyonyooka, Aamiin.
 
Pole na hongera kuweza ku-move on na mahusiano yako mapya.

Tayari Ushauri mzuri umetolewa na wadau hapo nyuma.

Kama ilivyoshauriwa, nami ningependa nikazie kwamba;

Ukusanye ushahidi wa maovu anayokufanyia iwe wewe ama wapenzi wako, then ukamripoti Kituo cha Polisi kilicho jirani nawe.

Lakini pia, unaweza kuhama Mtaa ili kuweza kukaa naye mbali zaidi
 
Back
Top Bottom