Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,029
Binafsi nakushauri yafuatayo;Salaam WanaJF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana β mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF β kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.
Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.
Narudi kwenye mada kuu...
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu β sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.
Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom β japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.
Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.
Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika β nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".
Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.
Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana β zote mbili β lakini bado habadiliki.
Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu β nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?
Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
TapeliπHatimaye sasa umekutana na mme sahihi .
Zama PM chap weka namba hapa binti ,mimi ndiye dawa ya wanaume wajinga kama hako kaex kako .
Sijisifii ila ngumi za kupiga niko sawa nina mkanda mweusi wa karate ,kuhusu sheria hapa ndiyo mahali pake .
Ila pia hela si haba si nimeajiriwa bwana ,nakuambia kuwa huyo mjinga atajuta kukujua nitapiga alafu niweke ndani hata mwaka .
Nathubutu kusema suluhu ya shida zako ni mimi kwakuwa naona umeteseka sana .
Anyway zifuatzo ni sifa zangu mwanaume shababi hapa .
Mfupi kiasi
Nina tumbo kubwa ila lenye kuleta heshima kwa jamii ya watu waliostaarabika .
Ni mshari na mgovi haswa kwa wakorofi kama hako kaex kako .
Siko tayari kushuhudia maonezi yoyote .
Nimeajiriwa na serikali tukufu ya Tanzania .
Nina usafiri wangu mzuri mno (corolla ) nzuri mkoa mzima hakuna mwenye nayo kama hii .
Si bahili haswa nikipenda kama hivi .
Jitahidi kuwahi Pm kwangu maana kuna wanawake wataanza kunisumbua kwa wasifu wangu mkubwa wa namna hii .
Asante ,karibu nikutetee bibiye .
Una uzoefu nao?Bonge la narcist wanatesa mno hao viumbe!
NdioUna uzoefu nao?
Kuna msemo wanautumia team KATAA NDOA kuwa kumuoa single mother ni mpaka waone tuta la baba mtoto.Salaam WanaJF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana β mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF β kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.
Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.
Narudi kwenye mada kuu...
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu β sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.
Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom β japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.
Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.
Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika β nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".
Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.
Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana β zote mbili β lakini bado habadiliki.
Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu β nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?
Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
Wananchi wanapaswa kuruhusiwa kumiliki silaha za moto ili kujilinda dhidi ya watu mafedhuli.Kuna msemo wanautumia team KATAA NDOA kuwa kumuoa single mother ni mpaka waone tuta la baba mtoto.
Sasa naelewa namna hao wababa wanavyoharibu mfumo wa maisha ya masingo maza
Tupe mkasa ilikuaje!!?na wewe ulitekekezwa na ujauzito na matunzo hamna!!?Ndio
Wala mimi case yangu ni tofauti ni mtu alikuwa narcist basi, kama unazijua tabia za narcist utanielewa!Tupe mkasa ilikuaje!!?na wewe ulitekekezwa na ujauzito na matunzo hamna!!?
Maana kila single mother Huwa wanasema hivi:-alikua Malaya sana,hatoi matumizi,Hana future n.k
Hahhahahaaha jamanii, sio rahisi hivyo mkuu!Kumbe hata anavyomiliki na kijidaia ni yule ex alivinunua na ndivyo vinamweka mjini na kujiona kajipata superwoman or miss independent!
Kina mama wengi ninwezi sana by nature yaani wengi,wanakuibia kwa mgongo wa kulea watoto mliozaa,kumbe wanatumia kwa starehe zao!!Wala mimi case yangu ni tofauti ni mtu alikuwa narcist basi, kama unazijua tabia za narcist utanielewa!
Hahhahahaaha jamanii, sio rahisi hivyo mkuu!
Hmm mimi tukishindwana baki na wanao aisee! Mambo yasiwe mengi kabisaa! Hukunikuta na watotoπKina mama wengi ninwezi sana by nature yaani wengi,wanakuibia kwa mgongo wa kulea watoto mliozaa,kumbe wanatumia kwa starehe zao!!
Na ikitokea umejua Siri za ujinga wake ndio maji utaita mma!!
Utasikia "Bora tuachane"
Akiwa ame tagert kusingizia watoto ili kumiliki mlichochuma pamoja!!
Ni vichekesho sana huku kitaaa!!
Idea yako nzuri sana ila kabla ya kuifikisha mbali kwa kuitangaza hakikisha umefukia mashimo yote na kufanya maintainance ya kutosha! Kuendesha app si mchezo..Zungumza moja kwa moja na mmiliki wa nyumba au chumba unachotaka kupanga! π π±
Usizunguke kwa madalali wengi, usipoteze muda kutafuta taarifa zisizo sahihi, wala usihangaike kuulizia nyumba moja baada ya nyingine.
Kupitia PataChumba, unaweza kutafuta nyumba na vyumba vya kupanga vilivyotangazwa kwenye mfumo, kisha kupata taarifa muhimu za chumba au nyumba unayoipenda na kuwasiliana moja kwa moja na mwenye tangazo.
Na kama wewe ni mmiliki wa nyumba au chumba, PataChumba inakupa nafasi ya kutangaza nafasi zako ili zifikie watu wanaotafuta sehemu ya kuishi.
π Tafuta chumba.
π’ Tangaza nyumba yako.
π± Wasiliana moja kwa moja.
PataChumba Daraja kati ya wanaotafuta nyumba na wenye nyumba.
π Anza kutumia PataChumba leo.
PataChumba β Pata mahali pako
PataChumba β jukwaa la kutafuta na kusimamia nyumba za kupanga kwa Kiswahili.patachumba-8fd9leim.manus.space
Duh. Inasikitisha sana. Pole kwa mkasa huo. Labda ushauri naoweza kukupatia, angalia namna ya kumdhibiti kisheria, tresspassing. Kama hatoi matumizi, ana haki gani ya kukuita mkewe?Salaam WanaJF,
Miaka ya nyuma niliwahi kuleta hapa tatizo kubwa lililokuwa linanikabili. Kwanza kabisa, naomba niwapongeze sana β mliniinua. Nilikuwa nimekata tamaa ya kuishi, nilihisi sina tena thamani. Lakini kupitia uzi mmoja tu nilioweka hapa, maisha yangu yalibadilika kabisa. Niliweza kusimama tena, kujijenga na kuendelea mbele. Shukrani za dhati kwenu wanaJF β kuanzia uongozi hadi wanachama wa kawaida.
Wito wangu: msibeze uzi wa mtu anayeomba msaada. Hamjui yuko katika hali gani kiakili au kihisia. Si kila mtu ana ndugu wa karibu, marafiki au majirani wa kuongea nao. JamiiForums kwa wengine ni kama familia ya mwisho ya kusikiliza.
Narudi kwenye mada kuu...
Yule mwanaume aliyebadilisha maisha yangu kuwa machungu, alikataa kunipa talaka. Nilijikuta katika maisha ya sintofahamu β sijui kama bado ni mke wa mtu au msela. Aliniacha nikiwa mjamzito na mtoto wake. Hata baada ya mtoto kuzaliwa, hakutoa msaada wowote. Nilijitahidi kuvumilia, nikavunjika moyo, lakini bado niliendelea kuwa na matumaini.
Hatimaye niliamua kumwambia: naomba talaka. Nilikuwa tayari kuwa single mom β japo najua kuwa kundi hili nchini linaonewa na kubezwa mara nyingi. Lakini yule mwanaume alikataa katu katu kuniacha. Hakuwa mume wala mlezi.
Baada ya afya yangu kuimarika (nilijifungua kwa C-section), nilienda BAKWATA kudai talaka. Alipoitwa mara kadhaa alikaidi, lakini baadaye alipoona naendelea kusisitiza, alisema bado ananipenda, ila anaendelea 'kujitafuta'. Kwa sababu hiyo isiyo na msingi, niliamua kujivua mwenyewe ndoa ile, nikarudisha mahari. Ndipo alipopata hasira na kuwa mtu mwingine kabisa.
Akageuka kuwa kama kivuli changu.
Nilipofungua duka, alianza kuja kila siku, akikaa karibu ili kuniangalia. Akagombana na wateja wa kiume waliokaa muda mrefu, akifanya vurugu zisizoisha. Biashara ikaharibika β nikalazimika kufunga. Nilipoanza biashara nyingine, hali ikawa ile ile. Nikipata mchumba au mpenzi, anawinda, anampiga au anamfukuza kwa vitisho. Moja aliyejitokeza kunichumbia alimpiga vibaya sana, akamwambia akae mbali na "mke wake".
Nina wasiwasi hata simu yangu ameihack. Sina amani naye. Hana muda wa kutafuta hela za kulea mtoto wake, lakini ana muda wa kunifuatilia kila mahali. Amenigeuza mateka wa maisha yangu mwenyewe.
Ametoa maneno ya vitisho, na ninamwona kama mtu ambaye yupo tayari hata kuniua. Cha kushangaza, mimi ndiye niliyemuacha, kwa amani, nikamrudishia kila kitu, lakini yeye bado ana hasira kali kwangu. Familia zimeshamshauri sana β zote mbili β lakini bado habadiliki.
Naombeni ushauri wenu wanaJF.
Mtu wa aina hii, anayenifuatilia, anayevuruga maisha yangu, anayewatisha wanaume ninaokutana nao, na anayenitia hofu kwa maisha yangu na ya mwanangu β nimfanyeje ili aache kunisumbua kabisa?
Niko tayari kwa mawazo yoyote ya kisheria, kijamii au kiusalama. Asanteni sana.
Kumbuka tutaWananchi wanapaswa kuruhusiwa kumiliki silaha za moto ili kujilinda dhidi ya watu mafedhuli.