kisana moja, Naamini haya nayo yanaweza saidia...
1. Epuka kutafuniwa. Ukipewa habari wewe unaichukua kama ilivyo na kuikumbatia.
2. Epuka ushabiki, siku zote tazama jambo free of emotions with a clear mind bila kujalisha ni kitu gani.
3. Penda sana kusoma, kusoma hakuhusu tu mambo ya Siasa, yale ambayo ni msingi hasa yale ambayo kwa namna moja ama nyingine huguswa na Siasa. Take note; Siasa kama siasa ni narrow, kinachofanya iwe pana ni yale mengi ambayo hufanywa kwa jina la Siasa.
4. Uwe na an open Mind. Kusikiliza pande zote hata kama zipo nyingi za entity yoyote ambayo unataka kuielewa, na kuzisikiliza kwa umakini ulio sawa na vile vile katika kufuatilia entity husika.
5. Jf is the best place ya kujifunza Uchambuzi, si lazima ukawa mchangiaji kwa muda. Unaweza kuwasoma wadau mbali mbali katika mada mbali mbali wanavyochambua hoja zao (iwe za kukubaliana ama kukataliana) na hivyo yaweza kuchangia wewe kuelewa na kuongeza kitu katika uchambuzi.
6. Amini na usimamie kile ambacho wewe unaamini huku ukiwa hodari kujihusisha mijadala hasa na wale ambao wapo tofauti na wewe kimawazo ili kujitafakari upya kile ambacho unaamini na kile ambacho unakijua (Ukiacha walau nafasi kidogo ya kubadili msimamo endapo tu hoja na msimamo wako umeonyeshwa si njia sahihi).
7. Na mengine mengi...
Kuna members hapa Jamvini wataalam wa Uchambuzi wa Mambo ya Siasa wakipata nafasi pengine wataweza kuongezea kwa manufaa ya wengi.
CC -
Nguruvi3,
Mchambuzi,
Mzee Mwanakijiji,
EMT,
Jasusi,
Mag3,
Rutashubanyuma,
Ngongo,
n00b,
Ben Saanane,
Mkandara, na wengine weengi.