Nifanyeje kuwasaidia hawa wanawake waliotelekezwa?

Wewe umejua wametelekezwa lakini hujui sababu za wao kutelekezwa!

Kiufupi ni kwamba amna mwanaume anaekimbiaga familia bila sababu..

kipindi kabla sijawa na familia niliwahurumia sana wanawake wanaopitia magumu lakini baada ya kuingia kwenye familia ndio nikagundua wengi waliyatafuta hayo maisha tena kwa gharama kubwa bila kujua kua yatakuja wagharimu!

Mimi nakushauri tu fanya sehemu yako lakini sio kumuaminisha kila mtu kua hao wanawake walitekelezwa makusudi!
 
Mkuu mwambie wewe labda atasikia,mie nimeambiwa ni mtoto
 
Huwezi msaidia mpuuzi.
Hana ndugu, hana Mungu wake,

kanuni kuu duniani;
Fata Mambo yako.

Yesu anasema: Kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe.

Biblia inasema; usijifanye unahuruma kupita kiasi kwa maana aliyejuu anayaona yote.

Waache wahenyeke akili iwakae Sawa.

Hao ndio ujanani Wanaringaga sana. huyavamia maisha kwa kutaka mambo makubwa wakati wao ni watu wa mambo duni.

Acha wahenyeke, hawakuanza wao.

Kuwasaidia watu waliopigwa na Mungu ni kutafuta laana.

Acha mambo yaende kama yalivyo.

Mungu wao atawasaidia kama hawezi kuwasaidia basi.

Wanawake wa hivyo wengi wakisaidiwa huzingua baadae. Nina mifano ya kutosha.

Hata Wanaume wa hivyo usiwasaidie.

Usisaidie masikini, wengi ni chanzo cha mikosi na laana kwako.

iwe Leo au kesho au miaka 20 ijayo.
 
sister ili mimba mpaka iingie inahitaji mzuka eeh
nlikua najua mbegu zikiingia tu basi mimba hiiiyooooo🙂🙂🙂
 
Hawa wanawake wananiuma sana unakuta mwanamke anachoma mahindi na mtoto mgongoni hadi saa nne za usiku, mwingine ni chinga anatembeza bidhaa barabarai na mtoto mgongoni huku mvua na jua ni yake [emoji24][emoji24][emoji24]
Hapo mtoto akifikisha miaka miwili ghafla utaona ana mtoto mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh mbavu zangu mimi
 
Mi nafikiri kama utaweza kufungua hiyo taasisi naona ingejikita kutoa elimu kwa wanawake waache kuzaa kama hawana ramani ya maisha. Mtu unaamua kuzaa huku huna cha kipato ili baadae uhurumiwe si ni kuendekeza ujinga huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zungumza nao kwanza, sikiliza kwa undani story zao. Jua wanaweza kufanya nini ili waondokane na hali hizo. Kutelekezwa sio mwisho wa maisha bali mtazamo wako ktk hali hiyo ndio yaweza kuwa mwisho wako.

Kuna watu unaweza kuhangaika kumsaidia aondokane na tatizo fulani kumbe yeye ndio tatizo, utaishia kuumia tu.
Nimejifunza kuwa siwezi kusaidia kila mtu, ila yule anayehitaji msaada wangu(namaanisha "ANAYEHITAJI") huyo nitamsaidia kadri niwezavyo.
 
Kabla ya kuwahurumia fatilia background zao kwanza, wengine inawezekana wamenyoshwa na maisha ila hapo kabla walikuwa hawashikiki. Hakuna mwanaume anaweza telekeza mke na watoto hivi hivi tu
Usiseme tu kirahisi kuwa "hakuna mwanaume" wapo sana tu, wewe kama hauwezi basi usijumuishe wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…