Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Ongea na mume wake ,na pia baba mwenye nyumba juu ya hio kero. Uwe bold, alternatively kama uchumi unaruhusu na moyo wa kutoa unao endelea,

Kwani huyo mke ni kabila gani?
 
Kula huyo mwanamke hadi alie utakuja kutushukuru pale kijiweni amekuona haujielewi dio maana ametuma watoto wake vigoli akupe kesi ya ubakaji
 
Wema haujakuponza bado, siku wema ukikutandika vizuri muda wa kula hautaweza hata kumkaribisha aliye karibu nawe.
 
Binadamu bhana! Yaani ududu wapigane wao, mapaja wapanuane wao, raha waone wao, watoe vijusi ambavyo hawawezi kuvihudumia, halafu wakuswekee mzigo
 
πŸ˜€πŸ˜€ Mkuu tatizo la kwanza ni wewe, la pili ni wew na la tatu ni wewe.
How comesπŸ€” unashinda nyumbani asubuhi upo mchana upo jion upo, ebu acha ujinga wahi job mapema jion nenda viwanja, rud saa 5, afu punguza mazoea na watu, mimi ukizoea kufanya jambo afu linanikera huo mchano nitakao kupa hutakaa urudie
 
Nilishawahi wafanyia hivo, wanapumzika siku 4 au 5.
Ya sita hawa hapa
Wakiwa wana gonga mlango usiwafungulir wala kuitikia we kaakimya tu na ukipika chakula waambie kimeisha, na wewe siku moja jifanye unaumwa na kuanza kuwaomba chakula chao unatakiwa uwaombe wiki nzima
 
Wasaidie kwa uwezo wako ukiwa huna waambie sina! Usichoke kuwasaidia ndo Maisha yalivyo,,! Kila kitu kina sababu zake unaweza kuta unavyowasaidia na wewe mambo yako ndo yanaenda! Au unahisi Tangu uwe unawasaidia kuna kitu kimepungua?
 
Hapo kuna Mambo mawili
mosi Wewe ni sehemu ya hyo familia πŸ˜†πŸ˜†
Pili, Unavyoendelea kutoa na kuwasaidia Hao watoto ndivyo Unavyabarikiwa..
Ila kama unataka kufanya maendeleo hyo nyumba Ama
 
Unaelewa chochote kuhusu Ubuntu ?

Wewe wasaidie, utalipwa maradufu na Allah.
 
Ushageuzwa mtunzi wa hiyo familia pia. Familia kubwa hyo ishawaelemea. Watoto watano 5 chumba kimoja pamoja na Baba na Mama Loh.. Wanaume kama maisha bado hayajakaa sawa kwanini kuzaa??
 
Aisee Kila kitu kina kiasi dada. Hata swadaka Ina kiasi pia.
Mtindo wa huyo Kila siku anakuja kukuomba eti umsaidie hapana aisee ni vibaya,hata dini hairuhusu kuomba omba hovyo.
Humu ndani wasikudanganye watu kuwa eti wasaidie tu utabarikiwa HAPANA HAPANA dini yenyewe haipendi tabia ya kuomba omba.
Na dini yenyewe inahimiza kutoa ukiwa na uwezo na USIIKALIFISHE NAFSI YAKO Yani umetoa huku masononeko.
Unawaendekeza hao dada,ushauri mzuri ni WA aina mbili,kwanza mwambie mumewe hata akifikiria vibaya shauri yake,pili uhame hapo hapakufai.
Sitaki kuamini kwamba nyumba ya karibu na kazini huo mtaa ni nyumba hiyo peke yake.
Hama hapakufai,hakuna Cha kusaidia sadaka Wala nini washakugeuza shamba la bibi wanajiendekeza.
Hata dini haipendi kuendekezana.
 
Asante sana mkuu.
Nashukuru kwa ushauri wako.
Nitahama soon!
 
Asante sana mkuu.
Nashukuru kwa ushauri wako.
Nitahama soon!
Mkiendelea hivi mtafikishana pabaya wivu wa kimaendeleo unaweza kuzuka mwisho chuki na ushirikina ukafuata.
Unachoeleza niliki experience na familia yangu pindi tunakaa Kigamboni kisiwani,jirani hadi njiti ya kibiriti anakuja kuomba kwako hadi sukari ya chai.
Hiyo siyo vizuri hata kidogo.
Msaada una kiwango pia hata unapoenda kuhamia jaribu kuweka mipaka usiruhusu watu wakuzoee kupitiliza,weka mazoea ya kawaida ya kijamii tu basi.
 
Imeandikwa
Ombeni nanyi mtapewa.
 
Sawa mkuu.
Nimekuelewa sana.
Asante sana
 
Kuna jambo la kujifunza wote hamuwezi kuwa matajiri au masikini MUNGU umneemesha mmoja ili awasaidie wengine kubali kutumika kama chombo Cha MUNGU kuwasaidia wengine kuliko kusaidiwa heri mkono mtooa kuliko upokeao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…